The House of Favourite Newspapers

Mayele Ampongeza Fei Toto kwa Kuifunga Yanga

0

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Fiston Mayele amempongeza kiungo wa Azam FC ambaye naye amewahi kukipiga Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kufunga goli la ushindi wa 2-1 kwenye mchezo dhidi ya waajiri wake wa zamani (Yanga SC) uliopigwa juzi Machi 17, 2024.

Mayele ambaye kwa sasa anaekipiga kwenye klabu ya Pyramid Misri, amempongeza Fei Toto kupitia kwenye post ambayo Feisal aliipost kwenye ukurasa wake inayoonyesha goli alilofunga kwenye mchezo huo na Mayele aliacha comment fupi “Hongera bro”.

Huu unakuwa mchezo wa tatu kwa Feisal kukutana na Yanga toka ajiunge na Azam FC na linakuwa goli lake la kwanza kuiwamba Yanga toka aondoke kwenye viunga vya twiga na Jangwani.

Leave A Reply