The House of Favourite Newspapers

Mayweather Amchapa Mkali wa ‘Mixed Martial Arts’ Mikuru Asakura Kwa KO – Video

0

Lejendari wa masumbwi duniani, Floyd Mayweather  asubuhi ya leo Jumapili Septemba 25, 2022 amemchapa mkali wa mixed martial arts mjapan Mikuru Asakura kwa KO ya raundi ya pili huko Japan.

Mikuru kuelekea katika pambano hilo alikuwa akinolewa na Seneta Manny Pacquiao, ambaye pia alikuwa ukumbini hapo kushuhudia pambano hilo.

Hili ni pambano la nne la hisani kwa Floyd Mayweather aliyestaafu ngumi mwaka 2017 akiwa na rekodi ya kucheza mapambano 50 ya ngumi za kulipwa bila kupoteza.

Matatu yaliyopita alimchapa Tenshin Nasukawa (2018), Logan Paul (2020) na Don Moore (2022).

Leave A Reply