The House of Favourite Newspapers

MB Dog Amiliki 30% ya Hisa Kampuni ya Oman

0

GABRIEL NG’OSHA | AMANI | Showbiz Xtra

LEGENDARY wa Bongo Fleva, Mohammed Mbwana ‘Mb Dog’ aliyewahi kutamba na Ngoma ya Si Uliniambia amefunguka kuhusu ishu ya kumiliki asilimia 30 ya hisa kwenye Kampuni ya Prominent Lines ya nchini Oman.

Akipiga stori na Showbiz Xtra, Mb Dog alisema kuwa, nje ya kazi ya muziki amekuwa akifanya kazi kwenye Kampuni ya Prominent Lines iliyoko Oman inayoshughulika na utengenezaji wa matangazo mbalimbali akiwa anamiliki hisa kiasi hicho.

“Nje ya muziki ninamiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni ya matangazo ya Prominent Lines ya Oman, kwenye muziki ‘soon’ nitaachia wimbo wangu wa Ash Ashu, nasuburi mipango ya uongozi ikamilike,” alisema Mb Dog.

 

Leave A Reply