The House of Favourite Newspapers

Mb Dog kuitambulisha video mpya Januari Mosi

0

3MB Dog akitoa vionjo vya wimbo wake mpya wa ‘Siyo Siri’ kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).1Mkurugenzi wa QS Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya King D iliyopo Sinza, Afrika Sana jijini Dar. Kushoto ni Direkta Abby Kazi, kulia ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Q-Chillah.
2Mhonda (kulia) akimkabidhi Direkta Abby Kazi kitita cha shilingi milioni ishirini kama ada ya kumsajili katika Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment.

MKONGWE wa Bongo Fleva, Mohamed Mbwana ‘MB Dog’ anatarajia kuangusha bonge la shoo la utambulisho wa video ya wimbo wake mpya uitwao Siyo Siri.

Akizungumza katika Hoteli ya King D iliyopo Sinza-Afrika Sana jiji ni Dar, Mkurugenzi wa Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda alisema uzinduzi rasmi wa video hiyo unatarajiwa kufanyika Januari Mosi, Mwaka huu katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar.

“Tumedhamiria kufanya shoo kali ya kuufungua Mwaka Mpya 2016 katika uzinduzi huo. Video imefanyika Afrika Kusini chini ya Direkta wetu wa kampuni, Abby Kazi ambaye naye tumemsajiri kwa dau la shilingi milioni ishirini.

“Itakuwa hatari maana tuna bendi mpya kabisa ambayo ipo mikononi mwa mkongwe wa Bongo Fleva Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ ambaye pia ni memba wa QS Mhonda J Entertaiment, utapigwa muziki live, niwasihi mashabiki wafike kwa wingi kujionea uzinduzi wa tofauti,” alisema Mhonda.

Kwa upande wake MB Dog alisema siku hiyo atawakumbusha mashabiki wake nyimbo zake za zamani na mpya ambazo bado hazijatoka sambamba na huo mpya wa Siyo Siri.

“Tutaimba Latifa, Si Uliniambia, Mbona Umenuna na nyingine kali kwa kutimia live band. Si ya kukosa, nitakuwa na Q-Chillah hakuna kitakachoharibika, zaidi itakuwa burudani baab’kubwa,” alisema Dog.

(Story/Picha: Issa Mnally, Erick Evarist)

Leave A Reply