The House of Favourite Newspapers

Mbappe, Neymar Wakalishwa Chini Kusuluhisha Bifu Lao

0
Taarifa zinadai Mbappe na Neymar Jr hawaelewani

KOCHA wa klabu ya soka ya Paris Saint-Germain Christopher Galtier amewakalisha chini Kylian Mbappe na Neymar baada ya kile kilichotokea wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Ufaransa dhidi ya klabu ya Montpellier ili kuondoa tofauti zilizojitokeza kati yao.

 

Dakika ya 42 ya mchezo huo PSG walipata penati yao ya pili ya mchezo ambayo ilizaa goli, penati hiyo ikipigwa Neymar licha ya Mbappe kumuomba amuachie apige penati hiyo.

 

Mbappe ambaye alikosa penati ya kwanza ya PSG dakika ya 22 ya mchezo huo hakuoneshwa kufurahishwa na kitendo kile cha Neymar kumnyima kupiga ile penati ya pili ili asahihishe makosa yake ya kukosa penati ya kwanza na kupelekea wawili hao kuvutana katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Kocha wa PSG Christopher Galtier

Kocha Christophe Galtier hakutaka kulifumbia macho jambo hilo hivyo aliwaita wawili hao na kufikia suluhu ya upigaji wa penati klabuni hapo. Walikubaliana kwamba katika kila mechi penati ya kwanza kupatikana itapigwa na Mbappe na iwapo itapatikana penati nyengine kwenye mchezo huo Neymar ndiye atakayehusika na penati hiyo. Hili lilifanyika ili kuepusha mgogoro huo mdogo kukua na kuwa tatizo kubwa baina ya wawili hao.

 

Siku ya jana Agosti 21, 2022 PSG waliichakaza klabu ya Lille kwa mabao 7-1 huku wawili hao wakionekana kutoonesha tofauti zozote kati yao.

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply