The House of Favourite Newspapers

MBARAKA AHUSISHWA NA MATOKEO MABAYA YA KAGERA

 

KITENDO cha Kagera Sugar kuwa na matokeo mabaya msimu huu, kimetajwa kuwa ni kuko­sekana kwa mfungaji mahiri ndani ya kikosi hicho kama alivyokuwa Mbaraka Yusuf ambaye kwa sasa anaitumikia Azam FC.

 

Mbaraka kabla ya kuihama timu hiyo, msimu uliopita aliisaidia ku­fanya vizuri ambapo alifunga ma­bao 12 huku timu hiyo ikimaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 53.

Kabla ya mechi za jana Jumapili, Kagera Sugar ilikuwa nafasi ya 14 ikiwa na pointi 18, ikiwa imefunga mabao 12 pekee ambayo msimu uliopita yalifungwa na Mbaraka peke yake. Kwa sasa Venus Ludovick ndiye kinara wao akiwa na ma­bao matatu akifuatiwa na Jafar Kibaya na Edward Christopher ambao kila mmoja ana mabao mawili.

 

Akizungumzia hilo, Maxime alisema: “Timu zetu hizi ndogo tunakuwa na changamoto nyingi sana hasa katika kuwaandaa wachezaji ambao watakuja kukusaidia, msimu uliopita tulikuwa na Mbaraka ambaye alikuwa analijua haswa goli, msimu huu hayupo kikosini kwetu.

 

“Sasa tunaendelea kumuan­daa mchezaji mwingine ili aweze kuwa kama yeye jambo ambalo ni nadra sana kulifanikisha kwa kiwango kile ukitakacho kwa sababu wachezaji wanatofau­tiana.

“Wenzetu timu hizi kubwa zina kila kitu na zina uwezo wa kumchukua mchezaji yeyote wanayemtaka, kwetu ni changa­moto, lakini tutaendelea kupam­bana, mechi bado zipo nyingi naamini tutafanya vizuri.”

Omary Mdose, Dar es Salaam

Comments are closed.