The House of Favourite Newspapers

FULL TIME: YANGA 3-1 STAND UNITED

FULL TIME

93′ Mchezo unaelekea kumalizika.

92′ Stand wanafanya shambulizi kali lakini wanakosa umakini wa kumalizia.

90′ Zinaongezwa dakika 3.

 

88′ Shangwe zimeamka kwa Yanga, sasa wanashangilia kwa nguvu.

85′ GOOOOOOOOL….. Yanga wanapata bao la tatu kupitia kwa Obrey Chirwa baada ya kuachia mkwaju mkali.

83′ GOOOOOOOL….. Stand wanapata bao la kwanza kupitia kwa Vitalis Mayanga baada ya kufanya shambulizi la kushtukiza.

80′ Mchezo umesimama kwa muda, kipa wa Yanga anafunga kamba ya viatu vyake.

77′ Mwamuzi anampa kadi ya njano Raphael Daudi wa Yanga kwa kuchelewesha muda.

 

 

77′ Mabadiliko upande wa Yanga, Ibrahim Ajibu anatoka, anaingia Emmanuel Martin.

73′ Chirwa anapata nafasi lakini anakuwa mzito kufanya maamuzi.

71′ Stand wamebadilika na kufanya shambulizi lingine kali lakini ubora wa kipa wa Yanga, unasaidia kuokoa.

69′ Stand wanapata faulo nje ya 18 ya Yanga, inapigwa inatoka nje.

66′ Stand wanafanya mabadiliko, Gambo anaingia, Mathiasi anatoka.

65′ Stand wanaamka na kushambulia lango la Yanga kwa mara nyingine lakini wanakosa umakini wa kumalizia.

 

63 Stand wand wanacharuka, wnafanya shambulizi kali, Rostand anauwahi mpira.

61′ Yondani wa Yanga anacheza faulo, mwamuzi anapuliza filimbi.

60′ Rostand amesimama, mchezo unaendelea.

59′ Kipa wa akiba wa Yanga, Kabwili anapasha misuli.

58′ Mchezo umesimama kwa dakika mbili, kioa wa Yanga Rostand ameumia.

56′ Stand wanapata kona mbili mfululizo lakini Yanga wapo makini kuokoa.

54′ Kasi ya mchezo imepungua, timu zinasomana.

 

53′ Stand wanapata faulo baada ya mchezaji wao kuchezea vibaya katibu na katikati ya uwanja.

51′ Ajibu yupo chini ameumia. Mchezo umesimama anatibiwa.

50′ Ndikumana anapiga shuti mpira unatoka inakuwa goal kick.

48′ Yanga wanapata kona, anaenda kupiga Ajibu.

 

47′ Mchezo umeanza kwa kasi.

Kipindi cha pili kimeanza.

 

 

MAPUMZIKO

47′ Mchezo unaelekea kuwa mapumziko, muda wowote kuanzia sasa itakuwa mapumziko.

46′ Chirwa anatengeneza shambulizi kali lakini mpira unatoka.

45′ Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.

45′ Stand wanaota mpira inakuwa kona.

44′ Shuti kali langoni mwa Yanga lakini kipa anaupangua mpira na unakuwa wa kurushwa.

 

43′ Maka wa Yanga anamiliki mpira, anaurudisha nyuma kwa Yondani.

42′ Ajibu anarusha mpira, unaokolewa na kuwa kona langoni mwa Stand United.

39′ Said Makapu anaonyesha kuwa mtulivu na kupiga pasi kadhaa.

38′ Stand wanaanza kucheza kwa kutumia nguvu nyingi.

 

 

34′ Beki wa Yanga, Gadiel Michael yupo chini anatibiwa, mchezo umesimama kwa muda.

33′ Ajibu anafokeana na beki wa Stand United.

30′ Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

29′ Stand wanapata kona, inapigwa inaokolewa.

 

26′ Yusuf wa Yanga ameumia, yupo chini akitibiwa, mchezo umesimama kwa muda.

22′ Rafael Daudi anamiliki mpira katikati ya uwanja.

20′ Yanga wanashambulia, Obrey Chirwa anapiga krosi lakini wanashindwa kuitumia vizuri.

18′ Ajibu anapiga kona fupi lakini Stand wanaokoa.

17′ Yanga wanapata kona.

13′ Stand wamepoteza kujiamini na Yanga wanaendelea kumiliki mpira.

Ibrahim Ajibu anaipatia Yanga bao la pili, akipiga shuti kutoka upande wa pembeni mwa uwanja.

11′ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

 

10′ Yanga wanapigiana pasi kwa wingi.

8′ Yanga wapo mbele kwa bao 1-0 na wanamiliki mpira.

Yanga wanapata bao la kwanza kupitia kwa Yusuf Mhilu, anapiga krosi kutoka pembeni ya uwanja inaingia moja kwa moja.

6′ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

4′ Juma Abdul wa Yanga anasaidia shambulizi lakini mpira uantoka.

2’ Yanga wanafika langoni mwa Stand, mpira unatoka inakuwa goal kick

Mchezo umeanza.

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

 

PICHA NA MUSA MATEJA

Comments are closed.