The House of Favourite Newspapers

MBASHA AELEZA ANAVYOTEKETEZA PESA KWENYE SUTI

Emmanuel Mbasha

MUIMBA Injili Bongo, Emmanuel Mbasha ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Hizo Habari Mbaya Sizitaki, baada ya kuonekana mara nyingi akiwa kwenye mavazi ya kisutisuti na kutokurudia suti hizo, amebanwa na kueleza jinsi anavyoteketeza pesa kwenye vazi hilo ambalo mwenyewe anadai humuweka smati zaidi.

 

Akifanya mahojiano na Risasi Jumamosi, Mbasha alisema kuwa yeye mavazi yake hajawahi kuvalishwa na mtu, huwa ananunua nguo kisha anaondoka dukani tofauti na wale ambao huvalishwa na maduka mbalimbali.

 

Tumsikie kwenye mahojiano hayo

Risasi: Mbasha unaonekana kuwa na suti nyingi na kila mara unakuwa umevaa mpya, je una ‘sponsor’ au unavishwa na mtu flani?

Mbasha: Ni kweli nina suti nyingi na sina anayenivalisha wala ‘sponsor’, unajua mimi napenda sana kuvaa, napenda ‘usmart’ na kunukia vizuri, naamini hata jamii imenizoea hivyo. Hapa kwenye suala la kuvaa huwa natumia pesa yangu.

Risasi: Duh! Kwa mwaka huwa unatumia shilingi ngapi kwenye vazi hili la suti?

Mbasha: Ukweli siwezi kuwa na hesabu ya haraka haraka ila najua kila suti nimenunua bei gani kwani mara nyingi natumia kuanzia laki moja na nusu mpaka laki tano, inategemea aina ya suti na kitambaa chake.

Risasi: Je, suti zote unazonunua huwa unanunua duka moja au tofauti. Je, unatumika katika kutangaza maduka unayonunulia?

Mbasha: Nikwambie tu uelewe kuwa mimi najivalisha kwa pesa yangu na kama sikununua dukani huwa nashonesha kwa fundi wangu maalumu ambaye huwa nampa laki tatu ananitafutia kitambaa na kunishonea, linapokuja suala la mavazi huwa sina mchezo, nateketeza fedha bila kujali.

 

Risasi: Umesema unatumia pesa zako, je mbali na uimbaji wa Injili unafanya kazi gani nyingine?

Mbasha: Mimi naimba Injili lakini pia nafanya biashara ambayo sipendi kuitaja hapa kwani inajiendesha yenyewe haihitaji promo.

Risasi: Kwa mwezi unarudia nguo mara ngapi?

Mbasha: Kurudia nguo kwangu ni mara chache sana, kwani kama ni suti moja naweza kuivaa mara mbili tu kwa mwezi lakini siwezi kurudia zaidi ya hapo kwani ninazo nyingi.

Risasi: Umekuwa ni mtu wa kukaa sana mahotelini mara kwa mara, je na suala hilo likoje kwani wapo wanaodai huna nyumba maalumu ndiyo maana unapenda kukaa hotelini.

Mbasha: Kila ukiniona hotelini mara nyingi nakuwa nimeandaliwa na watu walionialika, aidha kwenye vikao au kwenye shoo flani.

STORI: Hamida Hassan

Comments are closed.