The House of Favourite Newspapers

Mbeba Mizigo Kigogo Dar Alamba Mil. 300 Tatu Mzuka

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatu Mzuka,  Sebastian Maganga, akielezea jambo kwa wanahabari kabla ya kumkabidhi Abeid Hamis cheki ya Sh. mil. 300.
Abeid Hamis akielezea  alivyocheza na kuibuka mshindi.
Maganga akiwa na Hamis wakati wa kukabidhi cheki.
Hamis akiwa na (mfano) wa cheki yake.
Taswira ya hafla nzima ilivyokuwa.

TatuMzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini,  leo umemkabidhi mshindi wa kampeni ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai, mwaka huu  (2018) kitita cha Sh. milioni 300.

 

Abeid Hamis (28) mkazi wa Mbagala, Wilaya ya Temeke,  Dar es Salaam,  ndiye ameibuka mshindi wa Jackpot kubwa kuwahi kutokea nchini.   Amri hakushinda peke yake bali alichagua timu yake ya watu 10 ili kukamilisha timu yake ya watu 11 ambapo kila mmoja amepata milioni moja.

 

“Tumepata faraja kubwa kushuhudia Mtanzania mwenzetu akipata ushindi mkubwa kiasi hiki. Umetuandikia historia leo kwa sababu haijawahi kutokea nchini Tanzania mtu kushinda million 300,” alisema Sebastian Maganga, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TatuMzuka

 

Msimu huu wa SupaMzuka Jackpot watu wamecheza na kushinda na marafiki, na  Hamis alichagua timu yake iliyokuwa na: Mwanaidi Omary, Subira Issa, Jasmin Issa, Shufwaa Issa, Farhat Issa, Omary Issa, Amin Issa, Mwanaasha Omary, Agness Samwel na Magdalena.

 

“Mimi sijala vizuri, wala kulala tangu siku hiyo Jumapili. Kila saa nawaza kama ni ndoto ambapo baadaye nitaamka, lakini sasa naamini kabisa kwamba ni kweli nimeshinda, ” alisema Hamis na kuongeza: “Nina furaha sana pia kushinda na marafiki, najisikia kama wengi tumeshinda!”

 

Wakati huohuo, TatuMzuka imesema  imeanza kutoa mafunzo kuhusu mikakati na mbinu za kutumia na kutunza fedha inazotoa kwa washindi.

 

“Tangu alipopata ushindi wake, tumeanza kumsaidia kutafuta wataalamu wa masuala ya utunzaji na uwekezaji wa fedha ili waweze kumshauri namna nzuri ya kuwekeza fedha zake ili ziweze kumsaidia zaidi,” alifafanua Maganga

 

TatuMzuka wanaendelea kuwapa Watanzania fursa ya kuwa mamilionea kwa kucheza Tatu Mzuka kupitia M-PESA, TIGO PESA na AIRTEL MONEY.  Mshiriki ataingiza namba ya kampuni ambayo ni  555111 na baada ya hapo aingize namba zake tatu za bahati,  kisha aingize salio kuanzia shilingi 500 mpaka 30,000. Anaweza kushinda kila baada ya dakika 10, kila siku milioni 10 ambapo Jumapili hii kuna ushindi wa Sh. milioni 60.

STORI: MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.