The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Apanda Ndege Na Majina Ya Ngassa, Dante na Kaseke

0


MABOSI wa Yanga wameamua kumpa rungu zito kocha wao Mbelgiji Luc Eymael la kumfi kishia majina ya wachezaji wote ambao wanamaliza mikataba kisha kufanya maamuzi ya nani na nani kubakia kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao.

Mabosi hao walimfi kishia majina hayo kocha huyo kwa ajili ya kufanyia tathmini ya kina wakati akiwa kwao Ubelgiji kabla ya kufanya maamuzi ambapo majina ya wachezaji ambao wangebaki yalitarajiwa kutumwa Ijumaa iliyopita.

 

Miongoni mwa nyota ambao majina yao yanafanyiwa tathmini na kocha huyo kutokana na mikataba kwenda kumalizika ni Mrisho Ngassa, Andrew Vicent ‘Dante’, Deus Kaseke na Tariq Seif.

Habari ambazo Championi Jumatano, limezipata na kuthibitishwa na Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ni kuwa kocha huyo baada ya kupewa majina hayo anaendelea kuyachambua kabla ya kuwapa mabosi wake ambao anawahitaji wabaki kikosini hapo kwa msimu ujao.

 

“Kocha kabla ya kuondoka aliomba orodha ya wanaomaliza mikataba na akapewa na uongozi kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini yake nani na nani anawahitaji kwa msimu ujao. “Alitarajia kuyatuma majina ya wale ambao anawataka wabaki Ijumaa iliyopita lakini hakufanya hivyo, lakini bado uongozi unaendelea kumsubiria kuona kitu gani atakisema kisha kwa wale ambao watapendekezwa kubaki tutamalizana nao mara moja,” alisema Bumbuli.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Leave A Reply