The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji atua na mbinu kiboko kwa Mbabane

 

WAKATI kesho Jumanne Simba ikiwa ugenini kucheza na Mbabane Swallows ya Eswatini, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameweka wazi kwamba plani yake ni kuimaliza mechi hiyo mapema kwa kupata bao la dakika za nwanzoni ambalo litawachanganya wapinzani wao.

 

Simba kesho Jumanne watakuwa nchini Eswatini kwa ajili ya mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Af­rika baada ya ule mche­zo wa awali jijini Dar es Salaam kushinda 4-1.

 

Akizungum­za na Cham­pioni Ju­matatu, Mbelgiji huyo amesema kwamba licha ya kuelewa ugumu ambao upo katika mechi hiyo, hasa wakiwa ugenini, wamejipanga, am­bapo plani yao ni kupata bao hilo la mapema ambalo litachangia kwao kucheza kiutulivu.

“Tunajua kwamba tupo ugenini na haiwezi kuwa mechi nyepesi hata ki­dogo kwani wenzetu nao watataka kuonye­sha kwamba wapo nyumbani ambapo ni muhimu kuibuka na ushindi kwa upande wao.

 

“Kitu kikubwa ambacho tumepanga kukifanya ni kucheza kwa utulivu na kutambua kwamba tulipata mabao mengi kule nyum­bani, hivyo ni lazima tu­linde ushindi wetu. Kitu kikubwa tutakachofanya ni kutoruhusu bao kwetu lakini pia tutajitahidi tufunge bao la mapema ambalo litakuwa msaada mkubwa kwetu,” al­isema Mbelgiji huyo

SAID ALLY, Dar es Salaam

TID: “Wasafi Festival Inahitaji Mnyama kama Mimi”

Comments are closed.