The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji: Sasa Simba Ni Ushindi Tu

KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems ameweka bayana kwamba kwa sasa ameandaa mipango thabiti ya kuhakikisha kwamba kikosi chake kinapata matokeo kwenye michezo yao iliyobakia ya ligi kuu.

Mbelgiji huyo wikiendi hii atakuwa na kibarua cha kuiongoza Simba kupambana na Stand United kwenye muendelezo wa ligi ambao utapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Kocha huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa kwa sasa wana uhakika mkubwa wa kupata pointi kwenye mechi zao.

“Tulikuwa tunapata ushindi lakini mara zote siyo ule mkubwa ambao watu wanautaka kwa kiwango kikubwa, kwa sasa tuna kitu ambacho tumeandaa ili tuweze kufanya vizuri.

 

“Tunataka kushinda na hilo ndiyo jambo kubwa hapa kila mmoja analitaka, hivi karibuni nilikuwa nawaelekeza wachezaji ni nini cha kufanya kwenye michezo yetu ijayo na naamini kwamba watakifanya kazi kuanzia sasa,” alisema Mbelgiji huyo.

Na Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.