The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Simba Ataka Mabao 120

WAKATI kikosi cha Simba kikiendelea kujifua vilivyo huko nchini Uturuki kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo raia wa Ubelgiji, Patrick Aussems amewapa mtihani mzito washambuliaji wa timu hiyo akitaka mabao mara mbili ya yale ya msimu uliopita.

 

Aussems ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akichukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre amewataka washambuliaji timu hiyo kuhakikisha msimu ujao wanaongoza timu hiyo kufunga mabao mengi zaidi ya yale waliyofunga msimu uliopita.

 

Katika msimu uliopita Simba ilifanikiwa kufunga mabao 62 katika mechi 30 ilizocheza kwa hiyo kutokana na maagizo hayo ya Aussems kwa washambuliaji hao watatakiwa kufunga zaidi ya mabao 120 msimu ujao ambayo ni mara mbili zaidi ya yale ya msimu uliopita lakini sasa wakiwa wanatakiwa kucheza michezo 38. Akizungumza na Championi Jumatatu kwa njia ya simu kutokea nchini Uturuki, mshambuliaji wa timu hiyo, Mohamed Rashid alisema kuwa kocha huyo amefi kia hatua hiyo kutokana na mazoezi ya uhakika ya kuzifuma- nia nyavu ambayo ame- kuwa akiwapa- tia washambu- liaji wa timu hiyo.

Washambuliaji ambao wanatarajiwa kuwika msimu ujao ni  Mganda Emmanuel Okwi, John Bocco, Mnyarwanda Meddie Kagere, Adam Salamba, Mohamed Rashid pamoja na Shiza Kichuya. “Tunaendelea vizuri na kambi yetu huku na kazi iliyopo ni moja tu ya kujifua kwa nguvu na kila mchezaji anapambana kuhakikisha anakuwa fi ti lakini pia kumshawishi kocha ili aweze kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

 

“Lakini pia hivi karibuni kocha ametuambia kuwa kuwa msimu ujao anataka tuongoze timu yetu kufunga mabao mengi zaidi na ikiwezekana yawe mara mbili zaidi ya yale ya msimu uliopita kwa sababu anaamini uwezo huo tunao kuto kana na aina ya mazoezi ya kuzifumania nyavu ambayo amekuwa akitupatia.

 

“Aliwaambia kuwa kama msimu uliopita tulimaliza ligi tukiwa tumefunga mabao 62, basi msimu ujao tunaweza kufunga mabao mengi zaidi ya hayo, kama tutataka kufanya hivyo kwa kuwa pia michezo itakuwa mingi,” alisema mshambuliaji huyo mpya.

Stori na Sweerebert Lukonge, Championi Jumatatu

Comments are closed.