The House of Favourite Newspapers

SOLO THANG ADATA NA MAUA SAMA

Tokeo la picha la solo thang
Msafiri Kondo ‘Solo Thang’,

MWANAMUZIKI mkongwe katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, ambaye kwa sasa anaishi Uingereza hivi karibuni ameweka wazi kwamba anapenda sana muziki wa wanamuziki wengi wa kike Bongo lakini zaidi anamsikiliza Maua Sama.

Akipiga stori na ukurasa huu wa burudani dairekti kutoka ughaibuni, Solo alisema Maua anajua muziki pia ni miongoni mwa wadada wanaomkuna sana.

“Kiukweli ninapenda anachokifanya Maua Sama, ni mwanamuziki mzuri, ingawa nipo nje namsikiliza sana na anasikilizwa sana pia, lakini mbali na yeye wanamuziki wengine kama Diamond, Ally Kiba, A.Y, Fid Q, kazi zao zinatufikia na tunapata nafasi ya kuzisikiliza,” alisema Solo Thang.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.