The House of Favourite Newspapers

Mbeya City Uso Kwa Uso Na Singida Leo

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi jioni ya leo Jumamosi kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini.

 

Kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa, kutakuwa na mchezo kati ya vibonde wa ligi msimu huu, Singida United dhidi ya Wagonga Nyundo wa Jiji la Mbeya, Mbeya City FC.

Mchezo huo ambao utaanza majira ya saa kumi jioni ya leo Jumamosi, unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa kutokana na timu zote kutokuwa na matokeo mazuri msimu huu.

 

Mbeya City FC imekuwa ikisota kupata matokeo chanya kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema pindi ligi ilipokuwa imesimama ilimpa nafasi ya kukiandaa vema kikosi chake.

Comments are closed.