The House of Favourite Newspapers

MBEYA: Taarifa ya Serikali Kuhusu Moto Ulioteketeza Soko la Sido

0
Moto ulivyoteketeza Soko la Sido, Mbeya.

Natoa pole kwa wote walioathirika na janga la moto kwa wafanyabiashara soko la Sido. Soko la Sido lilianza kuungua saa 21.32 Hrs jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko la sido.

Pamoja na kutoa pole niwashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa ya kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara makubwa zaidi.

Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Mbeya imeunda kamati  ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha Moto huo .

Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana

Aidha vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu/watu uchunguzi huo bado unaendelea

Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu

Amos G.Makalla
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

 

Hatari! Moto Mkubwa Wateketeza Kabisa Soko la Sido, Mbeya

Leave A Reply