The House of Favourite Newspapers

Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuzindua Miradi ya Maendeleo ya Milioni 735 Jimboni Buchosa

0
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo akizungumza mara baada ya kupokea mwenge wa uhuru

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo amesema anafuraha kushiriki mbio za mwenge wa uhuru na kukiri kuwa hii ilikuwa mara yake ya kwanza  kuushika mwenge  tangu ulipozinduliwa hapa nchini.

 

Ameseme uwepo wa mwenge wa uhuru katika halmashauri ya Buchosa kutaleta manufaa na mshikamano ndani ya halmshauri hiyo sambamba na kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi hiyo.

 

Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake Julai 18/2022 kwenye Halmashauri ya Buchosa ambapo unatarajia kuzindua na kuweka mawe ya misingi kwenye miradi ya yenye thamni ya sh 735 milioni.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Sahili Gereruma amewakata wananchi kutumia fursa zilizopo hapa nchi kujipatia maendeleo sambamba na kushiriki zoezi la sensa litalofanyika Agosti 23 mwaka huu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga aametoa wito kwa  wananchi wa Buchosa kushiriki zoezi la Sensa litakalofanyika Agosti23 mwaka huu.

 

Leave A Reply