The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Upelelezi Kariakoo Aungana na Waislamu Kata ya Gerezani Kuhamasisha Uzalendo

0
Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi ya Ilala Dr. Ezekiel Kyogo.

 

MKUU wa Upelelezi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo, Dar, OC-CID Dr. Ezekiel Kyogo jana Jumamosi aliungana na Waislamu wa Kata ya Gerezani iliyopo Kariakoo jijini Dar, katika muhadhara wa kifamilia ambapo waliswali, kula pamoja na kuiombea duwa njema nchi na kuwakumbuka kwa dua waislamu wenzao waliotangulia mbele za haki.

Afande Kyogo akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

Katika hafla hiyo mashehe na viongozi wengine wa kidini na kiserikali walitoa mawaidha mbalimbali yaliyoendana na hadithi za Mtume Muhammad S.A.W katika kujenga tabia njema na uzalendo. Baada ya watu mbalimbali kuzungumza Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo, Afande Kyogo naye alikaribiswa kama mgeni mualikwa kwa ajili ya kutoa nasaha zake.

Afande Kyogo (mwenye kanzi na koti jeusi waliosimama) akiendelea kutoa elimu ya uzalendo.

 

 

Akizungumza kwenye hadhara hiyo, Afande Kyogo aliwasifu waandaaji wa hafla hiyo ambayo ilijaa maneno ya hekima na malezi bora kwa vijana na watu wazima waliohudhuria ambapo alisema;

Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji (kulia) akimpongeza afande Kyogo kwa elimu ya uzalendo aliyoitoa kwenye hadhara hiyo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wananchi Wazalendo Tanzania (TWWT) Octavian Mutayoba.

 

 

“Natumia nafasi hii kuwapongeza waandaaji wa hafla hii ambayo imejaa hekima za kumtukuza Mwenyezi Mungu. Mihadhara kama hii inapoandaliwa mara kwa mara inasaidia sana kudumisha uzalendo na kudumisha uzalendo ambao ndiyo mzizi mkuu wa amani na upendo. Mwananchi ni lazima uipende nchi yako kwa kuwa mzalendo, kamwe tusipoteze uzalendo kama wanavyofanya baadhi ya watu wasio na uzalendo kwa kufikia hatua ya kubadilishana debe la mchele na silaha.

 

“Unakuta mtu anaokota silaha badala ya kuisalimisha kwenye vyombo husika anaamua kubadilishana wahalifu kwa chakula au pesa hiyo bila kujali kuwa silaha mwisho wa siku itakwenda kuua ndugu zako au hata wewe mwenyewe. “Hiyo yote ni kukosa uzalendo ambao unasababishwa na kukosekana kwa mihadhara ya kizalendo kama hii.” Alisema.

 

Afande Kyogo akimalizia kuzungumza kwenye mkutano huo aliwaomba wakati mwingine wanapoandaa hafla nyingine kama hiyo wasikose kumshirikisha ili ikiwezekana ashiriki katika maandalizi. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji.

HABARI RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL

Leave A Reply