The House of Favourite Newspapers

Mbongo Fleva Anayeishi USA, Rhino The Don aibuka Tingisha

0
Rhino The Don, kwenye pozi

Mbongo anayegonga muziki wa kizazi kipya nchini Marekani (USA), Rhino The ameibuka tena na ngoma yake mpya iitwayo Tingisha ambayo ni audio na video.

 

Rhino The Don amefanya ngoma kadhaa zilizotamba akiwa na baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kama vile, Mr Blue na wengineo.

 

Akizungumza na mwandishi wetu kutoka USA Rhino The Don amesema ngoma yake hiyo aliyoifanyia nchini humo anaamini itabamba kona mbalimbali za ulimwengu kuanzia USA, Bongo na kwingineko.

Msanii huyo amewaomba mashabiki ulimwenguni kote kufuatilia kazi zake kwenye mitandao ya kijamii kwa jina la Rhino The Don na kuiangalia ngoma yake hiyo mpya iitwayo Tingisha ili wajionee mautundu ya kijanja aliyofanya kwenye kichupa hicho.

“Wapenzi wa burudani na muziki na video nzuri naomba wafuatilie kazi zangu ikiwemo ngoma yangu mpya iitwayo Tingisha ambayo mtazamaji atapenda kuendelea kuiona tu”. Alimaliza kusema Rhino The Don.

Leave A Reply