The House of Favourite Newspapers

Mbowe Aongoza Viongozi Chadema Kuripoti ‘Central’

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe (kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika wakielekea katika ofisi za kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi hao na wenzao wakielekea ndani ya jengo la kituo kikuu cha polisi.
…Wakiwa wamepumzika chini ya mti wakisubiri utaratibu wa kuingia kituoni.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho leo wamekwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa polisi kuhusiana na maandamano yaliyofanywa na chama hicho Februari 16 mwaka huu kwenda kudai hati za viapo kwa wasimamizi wa kura katika ofisi za wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Mbowe amesema atafuatana na viongozi wenzake sita walioitwa na polisi, isipokuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, ambaye yuko nje ya nchi.

 

Comments are closed.