The House of Favourite Newspapers

Mbowe Apata Pigo, Aanguka Ghafla, Akimbizwa Muhimbili

MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuanguka ghafla alfajiri ya leo Jumatatu, Juni 18, 2018, hii ni kwa mujibu wa wakili wake Jeremiah Mtobesya.

 

Wakili Mtobesya, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mteja wake alianguka leo akiwa nyumbani kwake, hivyo asingeweza kufika mahakamani kwa siku ya leo.

 

Akiwasilisha taarifa hiyo, Wakili Mtobesya ameeleza kuwa Mbowe ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi namba 112 ya 2018 amefiwa na kaka yake Henry Mbowe usiku wa kuamkia leo.

 

Naye Msemaji wa Chadema, Makene amesema; “Ni kweli Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mh. Freeman Mbowe amepatwa na shida ya kiafya asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwake, na amelazwa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Dharura. Tutaenelea kuwajuza.”

 

Aidha, awali Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiambia mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa Mbowe na wenzake wanane kusomewa maelezo ya awali PH na kwamba wamejiandaa na wapo tayari.

Comments are closed.