The House of Favourite Newspapers

MBOWE ASABABISHA KESI YA VIGOGO WA CHADEMA KUPIGWA KALENDA

Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee (kulia) akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kusikiliza kesi inayowakabili Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maedeleo (HADEMA) kwa sababu Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambaye ni mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo mahakama imeagiza kuhakikisha anafika mahakamani katika tarehe ijayo kinyume na hapo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

 

kesi hiyo ilikuwa ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na ilikuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).

 

Wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali Ph, lakini mshtakiwa, Freeman Mbowe na Ester Matiko hawapo mahakamani.

 

 

Kutokana na hoja hiyo, Mdhamini wa Mbowe, Greyson Selastine ameiambia mahakama kuwa Mbowe amefiwa na Kaka yake wa tumbo moja na msiba umesafirishwa kwenda Moshi.

 

 

Naye dhamini wa Matiko, Patrick John alisimama na kudai kuwa anaumwa yupo Dodoma na ameambiwa apumzike.

 

 

Hata hivyo, wakili Nchimbi alipinga taarifa ya mapumziko ya Matiko akidai nyaraka zilizowasilishwa ni batili.

 

 

Kutokana na hoja hizo, Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Juni 25 ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali na kusikilizwa hadi Juni 29,mwaka huu.

 

 

Watuhumiwa wegie katika kesi hiyo ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa,  na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

 

 

Vilevile Katibu wa chama hicho Dkt.Vicenti Mashinji, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

 

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio wa halali.

 

 

Comments are closed.