The House of Favourite Newspapers

Mbowe Kupangua Mawaziri Kivuli, Wanaomuunga Lipumba Kung’olewa

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema muda wowote kuanzia sasa atapangua Baraza la Mawaziri Vivuli na kuwaondoa wabunge wa CUF kutokana na baadhi yao kumuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, na baadhi ya waliokuwa viongozi wa CUF kuhamia ACT Wazalendo.

 

Hata hivyo, CUF kupitia kwa Magdalena Sakaya imesema ikitokea mabadiliko yoyote ya aina hiyo watamuandikia barua Spika kuomba ziwepo kambi mbili za upinzani bungeni, na hivyo stahiki za kambi ya upinzani zitakwenda katika makundi mawili.

 

“Lakini wakileta tatizo lolote sisi tuna haki, tutaandika barua kwa Spika kuwepo kambi mbili. Kwa hiyo stahiki za kambi za upinzani bungeni zitagawanywa mara mbili.” Amesema Sakaya.

 

Sakaya alizitaja stahiki hizo kuwa ni mfuko kwa ajili ya wapinzani unaowawezesha kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuajiri watu wa kuwaandikia barua.

 

Akijibu hoja hiyo, Mbowe amesema wanaweza kufanya wanavyotaka, ikiwa kanuni na sheria zitawaruhusu na kusisitiza kuwa wao (CHADEMA) hawawezi kushirikiana na chama ambacho hakiko katika ushirikiano wao.

Mbunge Atahadharisha Figisu figisu Uchanguzi Wenyeviti Mitaa

Comments are closed.