The House of Favourite Newspapers

Mbunge Ahoji Wimbi la Dawa za Kuongeza Nguvu za Kiume, Makalio – Video

MBUNGE wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM),  ameibua hoja wimbi la dawa za kuongeza nguvu za kiume na makalio nchini.

 

“Kuna ongezeko la matumizi ya dawa za nguvu za kiume, Serikali imetafiti nini tatizo la nguvu za kiume? Sababu nyingi ikiwemo Kisukari,Msongo wa Mawazo, zipo dawa hazina kemikali zitumike hizo, ushauri wanaotumia watumie zilizopitishwa na wataalam,” amhoji Mlinga.

 

Hoja hiyo imejibiwa na Waziri wa Ulinzi, Dr. Hussein Mwinyi (kwa niaba ya waziri wa Afya), akisisitiza wananchi kutumia dawa ambazo zimethibitishwa na Mamlaka ya Dawa na Chakula nchini (TFDA).

 

“Katika mwaka wa fedha 2017/18 TFDA ilipokea kutoka kwa watumiaji na watendaji wa afya taarifa 238 za madhara yaliyohisiwa kusababishwa na matumizi ya dawa ambapo tathmini zilionyesha kuwa ni salama na zinafaa kuendelea kutumika.

 

“TFDA haijawahi kupokea taarifa za madhara kuhusiana na kucha za kubandika kutokana na kukosekana kwa takwimu hizo, serikali haioni sababu ya kufunga saluni zote wala kuwachukulia hatua wanaotoa huduma hii.

 

“Kumekuwa na taarifa nyingi za dawa zinazoweza kukuza maumbile, wale ambao wanatoa taarifa hizi bila ya uthibitisho wanatakiwa wachukuliwe hatua, mpaka sasa hakuna dawa yoyote ambayo kitaalamu imethibitishwa na imepewa kibali kwa ajili ya matumizi kama hayo,” amesema Mwinyi.

VIDEO: TAZAMA MJADALA HUO

Comments are closed.