The House of Favourite Newspapers

Mbunge Aponda Sera za Trump

Mbunge wa Congress, Pramila Jayapal.

RAIS  Donald Trump wa Marekani ameshutumiwa na mbunge wa baraza la Congress,  Pramila Jayapal kuhusu sera zake za kuwatenganisha watoto na wazazi wao wanaokamatwa kwa kuingia nchini humo kiharamu.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, kuna shinikizo kubwa dhidi ya amri hiyo ya Trump ambapo watu wanataka watoto waliotengwa na wazazi wao, warejeshwe kuungana nao.

Watoto waliotenganishwa na wazazi wao.

Watu 600 walikamatwa jijini Washington DC Alhamisi, akiwemo mbunge huyo,  kwa kuandamana kupinga amri hiyo ya Trump ambapo miongoni mwa waliotaka amri iondolewe ni aliyekuwa mke wa Rais George Bush,  Laura Bush,   na Mwinjilishi Franklin Graham.

Comments are closed.