Mbunge Lijualikali Ahukumiwa Jela Miezi Sita

peter-1

Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Lijualikali.

Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Lijualikali amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, bila faini baada ya kukutwa na hatia ya kuwafanyia fujo polisi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

kilombelo

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Lijualikali na dereva wake, John Bikasa wamekutwa na hatia ya kukata utepe wa polisi na kuwafanyia fujo wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Kabla ya tukio hilo, Mheshimiwa Lijualikali, amewahi kuingia matatizoni na polisi, baada ya Machi Mosi, 2016, kukamatwa na polisi na kuswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi, Wilaya ya Kilombero kwa madai ya kuingia katika uchaguzi wa Baraza la Madiwani wilayani humo, wakati ikidaiwa kwamba hakuwa na sifa za kuingia.

Endapo hatakata rufaa na kushinda, uwezekano mkubwa ni kwamba mbunge huyo atapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge, kwa sababu kisheria, mbunge hatakiwi kuwa na historia ya kukutwa na hatia ya kosa lolote la jinai.

halotel-strip-1-1

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment