The House of Favourite Newspapers

Mbunge Mahawanga Awaonya Wanawake Na Mikopo Ya ‘Kausha Damu’, Awapongeza Wanavicoba

0
Mbunge wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Elius Mahawanga.

Dar es Salaam Mbunge wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Elius Mahawanga amewaonya wanawake na watu wengine wanaoona sawa kukopa mikopo ya mitaani maarufu kama kausha damu ambayo mwisho wa siku wanaishia kudaiwa kwa kudhalilishwa.

Mbunge huyo ambaye ana taasisi ya kusaidia wanawake alisema hayo kwenye hafla ya Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu ambayo ndani yake kuna vikundi vidogovidogo vya vicoba ambapo walikuwa wakifanya sherehe ya kupongezana na kugawana mapato ya mwaka 2023.

Akizungumza kwenye hiyo hafla Mbunge Mahawanga ambaye amekuwa mara nyingi amekuwa bega kwa bega kwenye harakati za wanawake haswa wa Jiji la Dar na mdau mkubwa wa kuhamasisha vicoba vya kimaendeleo amewaasa wanawake na watu wengine kujiepusha na mikopo ya wafanyabiasha wa mitaani wenye tamaa na kutumia shida zao kujinufaisha ambayo mingi siyo salama.

Amesema ameshapata malalamiko ya wananchi wengi sana wakilalamikia kudhalilishwa na wakopeshaji hao kufikia kuitwa mikopo ya kausha damu na majina mengine mabaya.

Hafla hiyo ilianza kwa sara na duwa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.

“Nawashauri wananchi haswa kinamama wenzangu kujiunga na vikundi vya vicoba na kujiwekea utaratibu mzuri wa kujiwekea akiba zenu na kujikopesha wenyewe kwa utaratibu mzuri mtakaojiwekea na kutatua changamoto zenu.

“Nakipongeza sana hiki kikundi cha FATA Vicoba Endelevu ambacho ndani yake kuna vikundi vidogovidogo vingi kwa jinsi wanavyoendesha taasisi hiyo bila migogoro yeyote na kila mwanakikundi unayeongea nae anakupa ushuhuda wa mafanikio baada ya kujiunga nacho”. Alisema mbunge huyo.

Mbunge Janeth Mahawanga akiserebuka na wanakikundi kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Hanifa Tarimo alisema kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2017, kama kikundi kidogo na kimezidi kukua kila kukicha kimekuwa mkombozi kwa watu wenye ndoto mbalimbali za kutimiza malengo yao ya kifedha.

“Hapa tuna wafanyabiashara, waajiriwa na watu kutoka kada tofauti ambapo wengi wamekuwa wakitoa ushuhuda wa kukuza biashara zao, kununua viwanja, nyumba, kujisomesha, kununua magari na mambo mengine mengi.

“Hivyo bado tunawakaribisha wadau wengine wanaotaka kujiunga nasi milango bado iko wazi wakiingia kwenye mitandao ya kijamii watapata mawasiliano yetu.    HABARI/PICHA :RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply