The House of Favourite Newspapers

Mbunge Prof Majimarefu Afiwa na Mkewe, Spika Atoa Pole

Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu ‘Profesa Majimarefu’.

Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu ‘Profesa Majimarefu’ leo Jumatano Juni 6, 2018 amefiwa na mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

 

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kifo cha mke wa mbunge huyo, kubainisha kuwa aliaga dunia saa 3 asubuhi.

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza ametoa pole kwa Profesa Majimarefu pamoja na familia yake.

“Ni kweli amefariki, tumepata taarifa hizo si muda mrefu leo na alikuwa amelazwa kwa muda mrefu katika pale Muhimbili ICU (chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum).

 

Maofisa wa Bunge wakiwa na Ngonyani wako pale wanaendelea kutoa msaada wa karibu kabla ya kuendelea na taratibu nyingine,” amesema Ndugai.

 

“Na kwa sababu huyu mama pia alikuwa ni diwani kule Korogwe, Bunge na halmashauri ya Korogwe vijijini tutashirikiana kwa pamoja lakini kwa sasa tunaendelea kuwasiliana na familia ya Majimarefu.”

Comments are closed.