The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo Akabidhi Mifuko 100 ya Saruji Kanisa Katoliki – Video

0
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo akikabidhi tani 5 za saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa  Katoliki Parokia ya Kome, Geita wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Viongozi wa dini na serikali wametakiwa kutembea pamoja ili kukemea maovu na kulinda utamaduni wa Mtanzania ambao ni tunu tuliyoachiwa na wazazi wetu.

Haya yamebainishwa na Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikra Maria Msaada wa Daima, Padre Japhet Masalu kwenye Misa ya Dominika ya Matawi iliyofanyika Parokia ya Kome, Geita wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Misa hiyo pia imehudhuriwa na Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo sambamba na kukabidhi tani 5 za saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Hii ni ahadi aliyoitoa wakati walipofanya harambee ya kuchangia ujenzi wa parokia hiyo ambapo ameitimiza.

Kwa upande wake, Shigongo amesema aliona ni vyema kutumia ahadi yake aliyoitoa ya kulitumikia kanisa.

“Ninaahidi nitashirikiana na waamini wa parokia hii katika masuala mbalimbali ya kulijenga Kanisa la Mungu, huu ni mwanzo tutaendelea zaidi,” amesema Shigongo.

Mmoja wa waamini wa Parokia ya Kome, Anastazia John amepongeza Shigongo kwa kutimiza ahadi yake.

Leave A Reply