The House of Favourite Newspapers

Mbunge CCM Ajiuzulu Wiki 3 Baada ya Kushinda Uchaguzi

0

MBUNGE wa Jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejiuzulu ubunge kuanzia leo Jumatatu, Agosti 2, 2021 kutokana na sababu za kifamilia.

 

“Amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia jambo ambalo chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM,” imeeleza barua hiyo iliyoandikwa na Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

 

Mbunge Faki alichaguliwa Julai 18, 2021 katika uchaguzi mdogo kufuatia aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Khatib Said Haji kufariki dunia.

 

Leave A Reply