The House of Favourite Newspapers

MBUNGE SAME MAGHARIBI AJA NA STAILI MPYA YA KUTATUA KERO

Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dkt. Mathayo David akizungumza jambo na wananchi wa jimbo lake.
Dkt. Mathayo akiendelea kuwahutubia jambo wananchi wa jimbo lake.
Kushoto mwa Mbunge Dkt. Mathayo ni mifuko ya saruji ambayo aliichangia wakati wa mkutano wake.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dkt. Mathayo David (kushoto) akikabidhi fedha kwa baadhi ya wawakilishi wa wananchi kwa ajili ya miradi mbalimbali za jimbo lake.

 

 

Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dkt. Mathayo David Mathayo ameendelea na ziara yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi katika jimbo lake huku akija na staili mpya ya kutatua kero za wananchi kwa mtindo wa papo kwa papo kukabidhi baadhi ya ahadi zake alizoziahidi kwa wananchi wa jimbo lake.

 

 

Licha ya kutekeleza ahadi alizoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Same Magharibi mbunge huyo amekuwa akitekeleza wakati mwingine kutoa fedha taslim  pale anapoombwa na wananchi wakata husika nje ya ahadi anazotekeleza katika kila kata.

 

 

Akizungumza na wananchi wa kata ya Vudee na Bangalala mbele ya mbunge huyo Diwani wa Kata hiyo, Ngomoi Ntarishwa, pamoja na kumshukuru mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi zote alizoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wanachi hao alisem.

 

“Ndugu bunge wananchi wa Vudee wanakushukuru sana kwa utekelezaji wa ahadi ulizoziahidi na umetekeleza, sisi wanannchi wa tuna imani kubwa na wewe hivyo pamoja na kuwa umetelekeza bado tuna changamoto kadhaa ambazo tunaomba pia utusaidie”alisema Ntarishwa.

 

 

Mbunge huyo ambaye licha ya kutekeleza ahadi za mabilioni amekuwa akitoa pia fedha zake zilizo nje ya ahadi kwa wananchi  wake wanapomlilia shida na kuhakikisha hawaachi hivyo na kuzitatua papohapo.

 

“Ndugu zangu leo nimekuja kutekeleza ahadi zote nilizoahidi wakati nilipokuja kuwashukuru kwa ushindi wa kishindo ambao mlinichagua, lakini nasikia kuna watu wanapitapita wakisema kuwa Mathayo hajarudi, hivi niwaulize swali ilani inatekelezwa ndani ya kipindi gani, si ni kwa miaka mitano? hivi mtoto akiaanza shule akafika kidato cha pili utasema basi kabla hajafika kidato cha nne? alihoji mbunge huyo.

 

Mathayo amewataka wananchi hao  kutokubali kurubuniwa na kuendelea kuwa na imani na chama cha mapinduzi ambacho kupitia Rais Dkt. John Magufuli kimeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wake tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.

 

Akiwa katika kata ya Vudee na Bangalala mbunge huyo ametekeleza ahadi zake kwa kutoa fedha taslimu na  saruji mifuko  350 kwa ajili ya ujenzi wa shule, zahanati, vyoo vya wanafunzi, mabomba ya maji, mabati 200, matanki ya maji, comyuta, mashine za photokopi, mipira ya kuchezea, key bord, nondo, meza na viti, huku akiahidi kuleta katapila kwa ajili ya ujenzi wa barabara korofi ya Kisesa,vyote kwa ajili ya kata ya Vudee.

 

Baadhi ya ahadi mpya alizozitoa na kuzitatua papo kwa papo katika kata ya Vudee ni kompyuta, mashine ya photokopi, jiko la shule ya sekondari masheka, mabati 30, na upande wa zahanati ya kiji cha kisesa bati 100.

 

Ombi jingine alilolitekeleza papo kwa papo katika kata ya Bangalala ni kukubali kutoa gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kata hiyo, kuleta katapila kwa ajili ya kutengeneza barabara za kata hiyo, tenki la kuhifadhia maji, ambapo pia ametoa fedha taslim kwa ajili ya kununua mipira ya maji 20 na nyinginezo.

Comments are closed.