The House of Favourite Newspapers

Mbuzi wa ajabu watikisa Dar

0

Mbuzi (2)Mbuzi hao wakirandaranda.

GLADNESS MALLYA NA GABRIEL NG’OSHA

DAR ES SALAAM: Dunia ina mambo! Mbuzi wanaosemwa kuwa ni wa ajabu, wanatikisa Jiji la Dar es Salaam, baada ya kuonekana katika maeneo mbalimbali wakijichunga bila mwenyewe kufahamika, lakini wakiwa hawaibiwi wala kubughudhiwa, Risasi Mchanganyiko lina mkanda wa kusisimua.

Mbuzi hao wamekuwa wakijiongoza wenyewe, wakila majani hadi kwenye matuta ya barabara zilizopo katika maeneo mbalimbali ya jiji, jambo linalosababisha minong’ono na simulizi kadhaa kwa watu. Jambo lingine linalowahusu mbuzi hao ni ukweli kuwa licha ya kuonekana wako peke yao usiku na mchana, lakini hakuna mtu yeyote anayewaiba, licha ya jiji hilo kuwa na idadi kubwa ya vibaka na wezi pengine kuliko mikoa yote nchini.

Mbuzi (1)Simulizi zinadai, mtu yeyote anayethubutu kuwaiba au kuwadhuru kwa namna yoyote, hupatwa na madhara, jambo linalowafanya kuogopewa. Baadhi ya maeneo ambayo wanyama hao wameshuhudiwa na gazeti hili wakijichunga bila kuongozwa ni Ubungo, Mbezi Beach, Tegeta na maeneo ya Viwanja vya Leaders vilivyoko Kinondoni. Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kuzungumza na baadhi ya wananchi wa maeneo tajwa kuhusu mbuzi hao.

“Mimi nilishuhudia watu wakiwapakia mbuzi hawa usiku mwingi, nilijua kwa vyovyote hao ni wezi maana mwenyewe hawezi kuja kuwachukua usiku, lakini sikujishughulisha nao kwa sababu hata mmiliki halali simjui. Lakini asubuhi yake nilipopita nikawakuta, nikapata hamu ya kujua kulikoni.

“Nilipoulizia, nikaambiwa eti wezi wale walikwenda nao huko Kisarawe mkoani Pwani, lakini walipotaka kuwashusha wakagoma, walitumia kila njia wakashindwa, wakaogopa na wakaamua kuwarudisha, cha ajabu walipofika eneo lao tu, kabla hata hawajashushwa walianza kuruka wenyewe kutoka kwenye gari,” alisema Emmanuel Juma wa Tegeta.

Naye Zuwena Hamis mkazi wa Ubungo alisema mbuzi hao wameshazoeleka, kwani wakati mwingine hutanda barabarani kiasi cha kuyazuia magari maana mtu akiwagonga tu, lazima apate ajali. “Ole wako umpige, utakiona cha moto, juzi walilala barabarani magari yakashindwa kupita na kufanya madereva wageuze kwani wanaho_ a ukimgonga mmojawapo hau_ ki Mkuranga,” alisema.

Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Gaston Mwakyembe ili azungumzie hatua zinazochukuliwa na jiji katika kuwadhibiti mbuzi hao kutokana na uchafuzi  wa mazingira, lakini simu yake ilirudisha ujumbe wa kuomba udhuru, akiahidi kupiga muda mfupi ujao. Hata hivyo, alipotafutwa tena baada ya saa mbili, simu hiyo haikupatikana kabisa.

Leave A Reply