The House of Favourite Newspapers

MC WA MSIBANI HAPIGIWI MAKOFI

Image result for COUPLES

SHOGAAA eeehh haya sasa sema mwenyewe, ulijifanya hodari wa kupakua kumbe kupika kwenyewe huwezi, haloooo eeeehhh na bado, mwaka ndo huooo unaisha endelea kumsifia mwanaume hendsamu wakati wenzako wanasifia kuwekewa pesa kwenye simu na benki, heee heeeeiyaaaaa!

 

Kuna wakati unaweza kuwa unapiga mihayo lakini kiziwi anayekutazama akahisi tu unampigia kelele, upo nyonyo? Wanakwambia kidole chenye busara ndicho chenye ishara na kama hujawahi kufundwa basi wee ni hasara! Unaloooo eeehhh!

 

Shoga baada ya udambwidambwi huo tuingie kwa kileee kilichonifanya niwepo hapa, siyo unanitumbulia macho na kujiuliza leo vipi tena Anti Naa anatuletea mambo ya MC na misiba, shuuuutuuuu! Kimbelembele tu kama kichwa cha treni, mbele twende nyuma twende!

 

Ukiniona nina furaha jua nimetunzwa mwenzenu, cha usiku na asubuhi nimekipata na kuridhika tena nahema kimyakimya, siyo unashangaa na kusahau kama shuka halina mfuko, utajibeeeebaaaa shoga! Wanakwambia kuvaa dera siyo kazi kazi kulishikilia ati! Weeeraaa weeeraaaa!

 

Leo nipo na wee unayeona ujanja kushinda kwenye TV kisa mitamthiliya, mchana kutwa kibarazani, usiku tamthiliya kazi zote unamuachia hausigeli, mumeo akija unajua atengewe chakula na maji ya kuoga basi inatosha, unasahau kuwa anahitaji chakula kingine cha usiku, weee naweee!

 

Nikisema hivi shoga namaanisha! Ushahidi ninao wa mashosti wengine ambao wameachwa hivihivi na wengine waume zao wameishia kuchepuka kisa tu kuweka uvivu kwenye chakula cha usiku. Sawa hatukatai shoga kama chafya ya mpishi haizimi moto lakini siyo kihivyo jamani!

Related image

Siku nzima hujaonana na mumeo kwa sababu za kazi, wewe mama wa nyumbani basi jitengenezee muda akirudi naye ajisikie kuwa ana mke, achana na kuwa bize na matamthiliya au umbeya wa kwenye mitandao ya WhatsApp na Instagram, niseme mara ngapi mnielewe kuwa mwanaume anahitaji kupetiwa?

 

Tangu lini mshereheshaji (MC) wa msibani akapigiwa makofi jamani! Ifike mahali tujitambue basi kama wanawake wa kweli! Tujue muda sahihi wa mume akirudi kazini tuachane na mambo ya kupita, simu za nini? Umbea wa nini? Tamthiliya za nini? Badilikeni! Baada ya kusema hayo, tukutane wiki ijayo shoga yangu! Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu!

Comments are closed.