The House of Favourite Newspapers

Mchengerwa Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Busega

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Veronica Sayore

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Veronica Sayore kwa kile alichoeleza kuwa amekuwa akipokea malalamiko dhidi ya Mkurugenzi huyo juu ya utendajikazi wake usioridhishwa.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano Serikali Ofisi ya ya Rais Tamisem Nteghenjwa Hosseah mapema Asubuhi ya Leo Septembe 22, 2023 imesema kuwa Waziri Mchengerwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi huyo kuanzia Leo ili kupisha uchunguzi.

Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita siku Moja, tangu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM Taifa Mary Chatanda akiwa anahitimisha ziara ya Siku Moja katika Halmashauri hiyo kumtaka Mkurugenzi huyo ajitafakari.

Chatanda alisema kuwa amesikitishwa sana na namna ya utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo ambavyo hauko vizuri kwenye Halmashauri hiyo ikiwemo mahusiano yake na wenzake.

” Mwambieni Mkurugenzi asimame vizuri, narudia tena Mwambieni Mkurugenzi asimame vizuri, hayuko vizuri…ashirikiane na wenzake, ashirikiane na Chama ili mambo yaende vizuri,”…

Mchengerwa pia amemwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEM kuunda timu ya uchunguzi wa mwenendo wa utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo pamoja na matumizi ya fedha za miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri hiyo.

Leave A Reply