MCHUNGAJI ‘ALIYEJI-SELFIE NA MUNGU’, AMTAKA MCH LUKAU AMFUFUE MANDELA

 MCHUNGAJI mmoja nchini Afrika Kusini, Paseka Motsoeneng, maarufu kama Pastor Mboro, ambaye alishawahi kudai kuwa alifika mbinguni na kupiga picha na Mungu (kwa kutumia simu – ‘selfie’) amempa changamoto mchungaji mwenzake raia wa Congo DR, Alph Lukau,  anayeishi nchini humo ambaye hivi karibuni alijinasibu kumfufua marehemu.

Mchungaji Mboro amefika mbele ya Kanisa la Mchungaji Lukau na kumuomba Mungu awasamehe wachungaji wote waongo huku akisema amefika kanisani hapo kwa sababu anaona injili ya Mungu inachezewa huku akimtaka kama kweli ana uwezo wa kufufua basi amfufue Muasisi wa Taifa hilo, Nelson Mandela.

 

“Nimefika hapa kujua ukweli, hii miujiza ni uongo na kama si uongo nipe kidhibitisho, wacha tuongee kama watu wa Mungu, hii siyo sahihi, kwa niaba ya wachungaji wote na watu wa Mungu, waongo wote tusamehe,” amesema Pastor Mboro huku akiwa pembeni ya gari lake la kifahari BMW i8.

Loading...

Toa comment