The House of Favourite Newspapers

KUTOKA BUKOBA: HILI NDO KABURI ATAKAMOZIKWA RUGE MUTAHABA

MAANDALIZI ya kumzika marehemu Ruge Mutahaba katika kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba yamepamba moto na ujenzi wa kaburi umeanza jana Alhamisi, Februari 28, 2019.

Siperatus Mbeikya ambaye ni mmoja wa wanafamilia amesema taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kupokea wageni kutokana maeneo mbalimbali.

Pia, amesema maandalizi hayo yamekwenda sambamba na kukubaliana na kikosi cha usalama barabarani sehemu utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu Ruge.

Pilikapilika zimeongezeka katika eneo la msiba ikiwa ni pamoja na kumwaga vifusi kwenye maeneo korofi.

Mwili wa Marehemu Ruge unatarajiwa kuwasili nchini leo Ijumaa jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo ambapo kesho Jumamosi utaagwa na wapendwa wake katika Ukumbi wa Karimjee kabla ya safari ya kuelekea Bukoba ambako utazikwa Jumatatu, Machi 4, 2019.

Rais Dkt Magufuli ametoa ndege ya Serikali kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Ruge Mutahaba na waombolezaji kwenda nyumbani kwao Bukoba kwa ajili ya maziko.

Comments are closed.