The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Kenya Afikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Ugaidi

0
Paul Nthenge Mackenzie (katikati) amefikishwa kizimbani huko Malindi tarehe Mei 2,  2023.

Mchungaji wa Kenya alifikishwa mahakamani sakikabiliwa na tuhuma za ugaidi.

Tuhuma hizo zinatokana na vifo vya zaidi ya watu 100 waliogundulika kuzikwa katika msitu unaoitwa “mauaji ya msitu wa Shakahola,” waendesha mashtaka walisema.

Nchi hiyo yenye Wakristo wengi imeshangazwa na kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki mwezi uliopita katika msitu ulio jirani na mji Malindi ulioko katika pwani wa Bahari ya Hindi.

Paul Nthenge Mackenzie, ambaye alijitangaza kuwa ni mchungaji alianzisha kanisa la Good News International, mwaka 2003 na anashutumiwa kuwachochea wafuasi kukaa na njaa hadi kufa ili waende “kukutana na Yesu”, alifikishwa kizimbani huko Malindi.

Chumba kidogo cha mahakama kilikuwa kimejaa ndugu wa waathirika, huku Mackenzie akiwa amevalia suruali yenye rangi ya kahawia, na koti lenye rangi ya pinki na nyeusi, alifikishwa kizimbani akiwa na na takriban nusu dazeni ya polisi pamoja na washitakiwa wengine wanane.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa muda mfupi, ilihamishiwa katika mahakama kuu iliyoko mjini Mombasa, mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya, ambako watuhumiwa hao watajibu mashitaka ya ugaidi, mwendesha mashtaka Vivian Kambaga aliliambia shirika la habari la AFP.

“Kuna mahakama (huko Mombasa) ambayo inashughulikia kesi za aina hiyo kwa mujibu wa sheria ya kuzuia ugaidi”, Kambaga alimwambia hakimu wakati alipokuwa akisiliza kesi hiyo huko Malindi, na kuomba ihamishiwe mahakama kuu.

Ezekiel Odero ambaye ni mwinjilisti tajiri na maarufu, pia anatarajiwa kufikishwa katika mahakama kuu ya Mombasa baada ya kukamatwa huko Malindi siku ya Alhamisi akihusishwa na kesi hiyo.

Mpaka sasa Jumla ya watu 109 wamethibitishwa kufariki, wengi wao wakiwa watoto.

Uchunguzi wa kwanza wa maiti za watoto tisa na mwanamke mmoja kutoka Shakahola ulifanyika siku ya Jumatatu

Imethibitishwa kuwa njaa ndiyo chanzo cha vifo hivyo , pamoja na kwamba waathirika wengine walikuwa wamekosa hewa. mamlaka ilisema.

ZAMARADI AFUNGUKA BAADA ya KUZINDUA TV YAKE – ”SIO KWAMBA NINA HELA, MUME WANGU HAKUNIACHA”…

Leave A Reply