The House of Favourite Newspapers

Meda: Diamond Jibu Barua Yangu

medda-3Ahmed Abdul, “Meda”.

Kama unamkumbuka dogo aliyefanya vizuri Afrika ya Mashariki mwishoni mwa mwaka 2014. Msanii wa kizazi kipya Ahmed Abdul, maarufu kama “Meda” Kwa tiketi ya wimbo wake Barua kwa Diamond anapata wakati mgumu baada ya kukosa cha kuwajibu mashabiki zake pale anapohojiwa kuhusu mahusiano yake na Record Lebal ya WCB Wasafi Classic Baby.

diamondDiamond Platnumz.

Meda amekuwa akikosa majibu ya moja kwa moja pale anapouulizwa kuhusu sanaa yake na uongozi wa WCB. Upo uvumi kuwa msanii huyo anabaniwa kuingia WCB pia zipo tetesi kuwa hakuna maelewano baina yake na wadau wa WCB.

Mwisho wa juma Meda alitinga ofisi za Globa Digital na kutegua mtego wa kitendawili cha maswali yaliyopo mtaani kuhusu mahusiano yake n a WCB;

ilikuwa hivi……

Mwandishi: Mambo vipi Meda?

Meda: Ahsante, safi tu brother.

Mwandishi: Karibu sana Global Digital.

Meda: Shukrani mkuu.

Mwandishi: Okay Meda moja kwa moja tuanze jitambulishe kwa watanzania.

Meda: Shukrani ndugu mwandishi mimi jina langu kabisa la kitanzania naitwa Ahmed Abdul maarufu kama Meda Classic. Meda ni jina linalofahamika kwa watu wengi Tanzania na  East Africa kwa ujumla. Jina hilo limepata umaarufu mkubwa pengine umaarufu ulionizidi. Nilitambulika kupitia wimbo wa “Barua kwa Diamond”. Ni wimbo wangu wa kwanza ulionifanya nitambulike kwa kila rika East Afrika.

Mwandishi: Mimi pia nimekufahamu kwa wimbo wa Barua kwa Diamond….

Meda: Sure.

Mwandishi: Mpaka ofisi imeamua kukutafuta ni kwamba imekuwa kimya tumeona WCB inaendelea kufanya vizuri, tunamuona Harmonize, Rayvanny na Mavoko ni watu waliokuja nyuma yako vipi upande wako umekwamia wapi ama kwanini upo kimya?

Meda: kwa mimi binafsi sina tofauti yoyote na WCB, sina tofauti na Naseeb wala sina tofauti na boss yoyote wa WCB lakini inawezena muda wangu sahihi wa kuingia WCB bado haujafika ama kuna ishu ipo katika uongozi au kuna uwezekano vipo vitu vingi ambavyo uongozi unavijua lakini mimi sivijui. Ila ninaamini uongozi wa WCB unanifahamau Unamfahamu Meda, unafahamu muziki wa Meda.

Mwandishi: Unataka kuniambia mpaka sasa haujasaini WCB!

Meda: Naam naam.

Meda anainamia chini anataka kulia…..

Unadhani ni kwanini mpaka sasa haujasaini WCB?

Meda: Kama nilivyo eleza awali kaka nimetengeneza image ya WCB ila sijui kuna kitu gani kati kati kinaendelea na kama kuna ishu yoyote naamini uongozi utakuja kunijza wakati ukitimu.. So mimi kama mimi nashindwa kupata image ya moja kwa moja kwanini mpaka leo sipo WCB. Ila nimetengeneza image ya wcb.

Unaonekana kama mwana WCB kwa kila kitu vipi umewahi kuwa mwanafunzi wa Lebal hiyo ama ni vipi kwanini upo Hivyo?

Meda: Inatokea mtu ananimbai nipo kama Daimond, Ipo tu hivi kaka automatic najikuta nakua hivi nadhani ni love na pia Naseeb ni role modal wangu.

Mwandishi: Unahisi Diamond anakupotezea?

Meda anashtuka kidogo..

Meda: Hapana kaka  sidhani kwani mawasiliano yapo mazuri, kila ninachofanya katika muziki wangu kupitia page zangu za katika mitandao ya kijamii kina uhusiano na WCB na pia Napata shout out kwa member wa WCB kaka watu wa Karibu na Naseeb.  Pia kwa upande wa Naseeb mwaka uliopita nilikuwa namawasiliano naye mazuri, nadhani sasa ni ubize brother anashughuli nyingi.

Mwandishi: Kwanini unadike Barua kwa Diamond si msanii mwingine kama vile Madee, Chegge ama msanii yoyote mwingine.

Meda: wau wengi walikuwa hawaelewi, Ile ni story ya kweli kaka haikuwa kick kama baadhi ya watu wanavyodhani. Lengo langu ni kuonekana kwa uongozi wa WCB. Naweza kusema Mungu alibarii hisia zangu katika wimbo ule kwani hata Naseeb aliweza kuufanyia promo katika kurasa zake katika mtandao.

Mwandishi: Je yapo mahusiano baina yako na member wa WCB kama Harmonize, Rich Mavoko na Rayvanny?

Meda: ndio kaka yapo mahusiano mazuri baina yangu na WCB members, ni marafiki zangu kama Harmonize tulikuwa tunakiutana Mazuu Record kipindi wote tupo katika zero stage. Wakati narekodi wimbo wangu nashangaa jiji Harmonize aliingiza sauti pia katika Wimbo ule.

Mwandishi: Unatathmini ni nini kitatokea endapo WCB watakupa kisogo wasikuhitaji katika record lebal yao.

Meda anaonesha hali ya kunyonyonyea.

Meda: Aiiiseh Effort zangu zote ni WCB kaka ni sawa na mtu aliyechimba madini miaka mingi na ameshayaona madini kasha anatokea mtu na kulifukia lile shimo kaka inaumiza sana. Bado nina imani na WCB.

Mwandishi: Katika Team ya WCB pale kuna wadau, marafiki na familia pia. Unahisi kuna mtu yoyote anaweza kuwa anachuki au umewahi kujibiwa vibaya na wadau wa WCB?

Meda: Hapana kaka nipo nao vizuri WCB wote kina Ricard Momo ni kaka zangu amabo huwa wananishauri vizuri juu ya muziki wangu.

Mwandishi: Unawaambia nini mashabiki wenye taharuki ya kujua hatima ya Meda na WCB?

Meda: Nadhani hii ni changamoto ambayo nakumbana nayo sana mtaani, nimewahi kumtumia ujumbe Diamond ujumbe wa picha ulionesha mawasiliano ya Djs wa mkoa wanahoji na wanataka kujua mahusiano yangu na WCB. Nakumbuka nilimtumia Diamond alionesha kuguswa na matakwa ya mashabiki.

Meda: Kitu ambacho kinaniuma kaka niliwahi kuzushiwa kuwa nimesema Daimond ameiba wimbo wangu, ile ishu ilikuwa hivi nilienda kutambulisha wimbo wangu kituo kimoja cha redio hapa nchini, sasa wakati natambulisha ulipigwa na wimbo wa Daimond basi mtaani yakazuka maneno kuwa nimelalamika eti nimeibiwa wimbo na Diamond.

Mwandishi: ulichukua hatua gani?

Meda: Nilifanya mahojiano na vituo vingi vya redio kukanusha uvumi huo.

Mwandishi: Shukrani Meda kwa muda wako nikutakie harakati njema za kuulngania muziki wako.

Meda: Shukrani kaka, Shukrani Global publishers.

Imeandaliwa na Leonard Msigwa na Salum Kim/GPL.

Comments are closed.