The House of Favourite Newspapers

Media Day: Wanahabari Walaani Vitendo vya Kunyanyaswa na Viongozi na Wanasiasa

0

Bi Salome Kitomari akizungumza wakati wa kongamano hilo.

Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Bi Salome Kitomari amelaani vitendo vya baadhi ya watalawa na wanasiasa kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwanyanyasa na kuwatesa waandishi wa habari pamoja na matukio ya kuvamia vyombo vya habari hali amabyo inatishia uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

  Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza.

Bi Salome amebainisha hayo wakati akitoa salam za Misa Tanzania kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Rais Magufuri wakati wa kilele cha siku ya uhuru wa vyombo habari duniani ambayo kitaifa yanafanyika jijini Mwanza.

Amesema kuwa takwimu za waandishi wa habari wasio na mipaka duniani na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) zinaonyesha kuwa zaidi ya waandishi 100 wameuwawa dunaiani kote kipindi cha mwaka jana pekee.

Theophil Makungaakizungumza.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Vyombo vya Habari Tanzania, Theophil Makunga amesema maadhimisho hayo yatumike kuangali hali halisi ya waandishi wa habari ilivyo kutokana na vitishwa kuzuiliwa kufanya kazi zao kitu ambacho kinawanyima uhuru wa kufanya kazi zao.

Hata hivyo  ameongeza kuwa kwa sasa baadhi ya viongozi wa umma na makundi mablimbali yameibuka na kuanza kuwanyanaysa, kuwapiga,kuwatishia kuwauwa waandsihi wa habari hali ambayo inaweze kuatarisha usalama wan chi na kupoteza uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

Leave A Reply