The House of Favourite Newspapers

Meridian Bet, Lions Club Zasaidia Matibabu Ya Macho Bure

0
Meneja Uendeshaji wa Meridian Bet, Carlo Njato akizungumza jambo .

Kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet na klabu ya Lions, zimesaidia kampeni ya upimaji, matibabu na ushauri nasahaa ya magonjwa ya macho, sukari na shinikizo la damu, yaliyotolewa bure  kwenye Hospitali ya Polisi Kilwa Road, Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ililenga pia kutoa miwani bure kwa wagonjwa ambao madaktari waliwataka na matatizo ya macho  baada ya vipimo ambapo mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam walijitokeza.

Baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu ya bure.

Mganga mkuu wa Hospitali hiyo na Mkuu wa kikosi cha aAfya cha Polisi Nchini, Dk Hussein Yahya alisema muitikio wa Watanzania waliojitokeza kupatiwa huduma hiyo umekuwa mkubwa tofauti na ilivyotarajiwa.

Hadi saa 3 Asubuhi, watu 456 walikuwa wamejiandikisha kupatiwa huduma hiyo wakiwamo watoto na wazee, huku Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi, Kihenya Kihenya akiwaomba wadhamini hao, kampuni ya Meridian Bet na klabu ya Lions, kampeni hiyo kuwa endelevu.

“Meridian Bet na Lions club wameonyesha njia, natamani kampeni hii iwe endelevu,” alisema ACP Kihenya ambaye alitunukiwa nishani ya ugavana na kuwa balozi wa Lions Club.

Alisema wadhamini wa kampeni hiyo, kampuni ya Meridian Bet na klabu ya Lions wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kujitoa kwao katika jamii.

Meneja Uendeshaji wa Meridian Bet, Carlo Njato alisema wameamua kusaidia kampeni hiyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya.

“Tumeleta dawa, vipimo vya sukari, thermometer, miwani za jua na za kuonea na vifaa tiba mbalimbali ili usaidia kampeni hii,” alisema Njato.

Alisema hiyo ni mara ya tatu kwa kampuni yao wakishirikiana na Lions Club kusaidia jamii yenye uhitaji. Tulifanya hivi kwenye hospitali ya wazee Kinyerezi, pia wakati wa maadhimisho ya ugonjwa wa kanda duniani, tulitembelea na kuwafariji wagonjwa katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Dar es Salaam.

Alisema ushiriki wao kwenye kampeni ya matibabu ya macho katika hospitali ya Polisi Kilwa Road ni muendelezo wa kampuni kurudisha kwa jamii, lakini pia wanaunga mkono juhudi ambazo Serikali imekuwa ikifanya katika sekta ya afya nchini.

Gavana wa klabu ya Lions Tanzania, Moiz Bakari alisema klabu yao imekuwa ikijitoa kwa jamii na hiyo ni sehemu ya majukumu wanayoyafanya.

Wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi, Kihenya Kihenya (kushoto) baada ya kupanda mti wa mwembe kama ishara ya kutambua mchango wao.

Alisema klabu yao nchini Tanzania ina wanachama 660 ambao wamekuwa wakijitoa na kusaidia jamii yenye uhitaji katika nyanja tofauti ikiwamo ya afya, elimu na masuala mengine ya kijamii.

“Tunatamani watu wengi zaidi wajitokeze na kujiunga na klabu yetu kwa ajili ya kujitolea na kufanya kazi za jamii,” alisema.

Leave A Reply