The House of Favourite Newspapers

Meya Ubungo Akarabati Soko La Shekilango

0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akikagua soko la Soko la Shekilango Kata ya Ubungo.
Akizungumza na wafanya biashara na wananchi katika soko hilo.

Dar es Salaam: Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, leo amefanya mkutano na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango Kata ya Ubungo ili kuweka makubaliano ya kuanza ukarabati wa soko hilo.
Ukarabati huo umelenga kuliweka Soko la Shekilango na masoko mengine ya Manispaa ya Ubungo katika hali nzuri na ya kisasa ili kuongeza mapato kwa halmashauri.


Akizungumza katika mkutano huo, Meya Jacob amesema: “Maboresho ya soko hili yametengewa Sh. milioni 50 ambazo ni mapato ya ndani ambayo yaliyotokana na kodi zao na mpaka sasa fedha zipo kwenye akaunti ya kata.”
Meya Jacob amesema kuwa, maboresho hayo yataanza baada ya siku 7 kuanzia leo na yatachukua siku 14 kukamilika ambapo wafanyabiashara waliopisha marekebisho hayo watarudi sehemu zao za biashara kama awali.


Amesema mara baada ya wafanyabiashara kurejea maeneo yao, makubaliano ya ushuru yatakuwa kati ya Manispaa ya Ubungo na mfanyabiashara na siyo tena mfanyabiashara na walanguzi wa maeneo.
Kwa kufanya maboresho hayo ya soko, Meya Jacob atakuwa ametimiza ahadi yake aliyotoa alipokuwa akigombea udiwani mwaka 2015 katika kata ya Ubungo.


Aidha, meya huyo amesema Manispaa ya Ubungo imetenga Sh. Milioni 550 kukarabati na kuboresha masoko yake yote 10 katika mwaka 2017/2018 likiwemo Soko la Urafiki.

(PICHA/ HABARI: SIFAEL PAUL/GPL)

Leave A Reply