The House of Favourite Newspapers

Mfanyabiashara Maarufu PCK Atoa Msaada kwa Binti Aliyetumikishwa Kingono Afrika Kusini

0
Leyla Thysia akikabidhiwa pesa na Mtangazaji wa Kipindi cha Mapito Zaliam Adam, kiasi cha shilingi 300,000 kama msaada kutoka kwa PCK

PROMOTA na Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Patrick Christopher maarufu kama (PCK) ameguswa na mkasa wa binti Layla Thysia aliyesafirishwa na Kwenda kutumikishwa kingono nchini Afrika Kusini ambapo ametoa msaada wa shilingi Laki Tatu za kitanzania 300,000/= ili ziweze kumsaidia katika mahitaji yake.

 

Katika kipindi cha Mapito kinachorushwa na Global TV pamoja na 255globalradio, Layla alielezea mkasa mzima na sababu za yeye kwenda kutumikishwa kingono nchini Afrika Kusini kuwa zilizotokana na ndugu kudhulumu mali zote za wazazi wake baada ya kufariki ndipo akaishia kuhangaika mitaani kabla ya kushawishika na kwenda nchini Afrika Kusini ambako alijikuta akitumikishwa kingono.

Mfanyabiashara maarufu na Promota Patrick Christopher maarufu kama PCK

PCK ambaye ni mdau mkubwa wa kipindi cha mapito na ambaye amekuwa na desturi ya kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye changamoto mbalimbali za maisha ametoa msaada huo kama sehemu ya hamasa kwa kuunga mkono kufufua matumaini mapya ya watu wanaopitia changamoto mbalimbali za maisha.

Leave A Reply