Rufaa Kupinga Hukumu ya Kifo Mkoani Mara Yabatilishwa, Ushahidi wa Rufaa Ni wa Uongo
MAHAKAMA ya Rufaa Mkoani Mara imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na mtuhumiwa Matiko Chandruku kwa jina maarufu Kehu, kupinga hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumbaka hadi kumuua mtoto wa miaka saba, Marma Furahini.
Mahakimu Gerald Ndika, Winfrida Korosso na Omar Makungu walifikia uamuzi huo baada ya kuunga mkono hukumu ya kifo cha kisheria iliyotolewa kwa Chandruku(Mtuhumiwa) na Mahakama Kuu. “Sisi, kama mahakimu wa mahakama, tumeridhika na mashtaka dhidi ya Matiko, mahakama ya mwanzo ilitoa hukumu ya kifo kwake baada kujiridhisha mtuhumiwa anaumri wa miaka18” walisema.
Wakati wa kusikilizwa kwa rufaa hiyo, wakili wa upande wa Mtuhumiwa alilalamika pamoja na mambo mengine kwamba maelezo yaushahidi yalitolewa kimakosa ambapo mtuhumiwa alihukumiwa kifo isivyostahili kwa sababu alikuwa chini ya umri wa miaka 18.
Mahakama ilifanya uchunguzi wa hukumu kwa mujibu wa kifungu cha 320 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambapo upande wa mashtaka ulifanikiwa kuleta mashahidi wanne ambao walithibitisha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na umri wa miaka kumi na minane na miezi kadhaa.
Kwa mujibu wa mahakimu, pia ilibainika kupitia uchunguzi huo kwamba kadi ya kliniki iliyotolewa ilighushi umri wa mtuhumiwa kwa sababu inamtaja alizaliwa Julai, 2003 kwa jina la Mkani Marwa ambao ni uwongo na ushahidi wake haukuzingatiwa.
Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.