The House of Favourite Newspapers

Mganga Ampa Ujauzito na Kumuoa Binti Yake wa Miaka 13

POLISI Wilaya ya Mpigi wanamshikilia mzee Vicent Ssenonga mwenye umri wa miaka 69 ambaye ni mganga wa kienyeji katika Kituo cha Polisi Buwama kwa kumpa ujauzito binti yake wa kumzaa mwenyewe.

 

Polisi wamesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa mzee huyo anamnyanyasa binti yake huyo ambaye amemgeuza kama mke wake. Walidai alianza kufanya naye ngono tangu akiwa na miaka 13 mpaka sasa ana umri wa miaka 20, huku wakiwa wamezaa watoto watatu.

 

“Anadaiwa amemuoa, anamtesa binti yake mwenyewe, hampi chakula na huduma za afya, hatukuweza kuvumilia na kwenda kumchukua huyu mzee. Tumeambiwa kuwa amemtumia huyu binti kwa miaka 7 sasa tangu akiwa na miaka 13, na tunachunguza taarifa kuwa amemuambukiza HIV”, – Jospeh Kakama, Afisa Polisi wa zamu katika Kituo cha Polisi Buwama.

 

Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji, Robert Ssemuju amesema mganga huyo alikuwa akiishi na binti yake huyo pekee, baada ya kuwapa talaka wake zake sita, na watoto wake kutawanyika kutafuta maisha huko Kampala na sehemu zingine.

 

“Ssenonga amekuwa akimtishia huyu binti asiseme chochote kwa watu, lakini kutokana na afya yake ambayo inadhoofu kila siku, ameamua kutuambia na kuamua kuweza kumsaidia yeye na hawa watoto watatu”, alisema mwenyekiti wa kijiji.

Mambosasa: Abdul Nondo Alikwenda Iringa kwa Mpenzi Wake

Comments are closed.