The House of Favourite Newspapers

Mgonjwa Apasuliwa Ubongo Kimakosa

 

WAZIRI wa Afya Kenya, Sicily Kariuki ampa likizo ya lazima Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, Lily Koros ili kupisha uchunguzi baada madaktari wa mfumo wa fahamu kumfanyia upasuaji wa ubongo mgonjwa ambaye hakustahili.

 

Kisa hicho hicho cha kumfanyia upasuaji wa ubongo mgonjwa ambaye siye, kilitokea wiki iliyopita na kushangaza wengi ambapo jana ilikuwa siku ya mwisho kwa Maofisa wa Matibabu ambao walihusika, kueleza ilikuwaje hadi kosa hilo likatokea.

 

Taarifa ya Bi Koros iliyotolewa juzi Alhamisi ilieleza maofisa wanne wa matibabu walikuwa wamesimamishwa kazi, akiwemo msimamisi wa usajili ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa ubongo. Wengine ni muuguzi aliyekuwa akisimamia wodi, muuguzi wa kupokea wagonjwa kwenye chumba cha kufanyiwa upasuaji na ofisa wa kuwatia ganzi wagonjwa.

Comments are closed.