The House of Favourite Newspapers

Amtaka Mwakyembe Kuwashughulikia Nandy, Bill Nas

 

MHADIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Mshauri wa Masuala ya M,ahusiano Dkt. Chris Mauki amefunguka kuhusu skendo ya wasanii wa Bongo Fleva, Nandy na Bill Nas kufuatia kuvuja kwa video yao wakijiachia faragha.

 

Dkt. Mauki ameitaka Wizara inayoshughulikia masuala ya sanaa ichukue hatua dhidi ya wasanii hao ili kulinda maadili na nidhamu katika jamii ya Tanzania hususani kwa wasanii ambao ni kioo cha jamii ili iwe funzo kwa wasanii wengine na watu wengine katika jamii.

 

“Mheshimiwa Waziri Mwakyembe, Naibu Waziri pamoja na Baraza la Sanaa chini ya ndugu Mungereza. Tutaiona nia yenu ya dhati kabisa kwenye kudumisha maadili na nidhamu katika jamii na hususani kwa wasanii ambao wanajiita “kioo cha jamii” pale ambapo hamtoinyamazia hii hali ya kuanikwa mitandaoni matukio ambayo kiuhalisia yalihitaji privacy.

 

“Ninasimama sehemu ya ndugu zao hao wahusika, sehemu ya wazazi wao, sehemu ya wadogo zao, na wengine wengi ambao waliwaona kama role models wao. Kulikoni majukwaani tuwaone kama vioo vya jamii na huku nyuma mitandaoni mnaiharibu kabisa ile picha mliyoichora machoni pa watanzania?” amesema Mauki.

 

Aidha, Dkt. Mauki ameisitiza kwamba, kama ilivyoenea katika public basi jamii ijulishwe katika public ni hatua gani za kinidhamu zinafuata na onyo kwa wengine wenye fikra finyu na chafu kama hawa wanaohalalisha tabia za kingono mitandaoni. Ameeleza kwamba, masikio ya wenye akili na hekima yanasubiri kusikia kutoka kwenu viongozi.

Comments are closed.