The House of Favourite Newspapers

Mhubiri Mashuhuri Duniani Kufanya Tukio Kubwa la Utamaduni Dar es Salaam

0
Mhubiri Gurdev Sri Sri Ravishankar

MHUBIRI mashuhuri kutoka nchini India, Gurdev Sri Sri Ravishankar, ambaye pia ni Balozi wa Amani duniani atawasili nchini Tanzania Agosti 25, 2022 na siku hiyo hiyo kuhudhuria tukio la Utamaduni wa India na Tanzania jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikitano wa Julius Nyerere kisha kuhutubia dunia akitokea Tanzania.

 

Bw. Gurdev ambaye taasisi yake ya Art of Living ina matawi katika nchi 156 dunia anasifika kwa mahubiri yake kuhusu amani, kuhimiza masuala ya utamaduni na mazoezi kwa afya na mihadhara yake hutazamwa na zaidi ya watu milioni 500 duniani. Kwa ziara hii ya Afrika atatembelea nchi nne tu ikiwemo Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Dkt. Hassan Abbasi

“Anakuja Tanzania kuungana mkono pia Royal Tour na atafanya ziara maeneo mbalimbali, ataendesha tukio la utamaduni, atatazama filamu ya Royal Tour akiwa na ujumbe wake na atafanya mikutano na wafanyabishara wa Tanzania na India kwani taasisi yake ya Art of Living pia husaidia nchi kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali,” alisema Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Dkt. Hassan Abbasi, akiambatana na Balozi wa India hapa nchini katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam leo Agosti 23, 2022.

Leave A Reply