The House of Favourite Newspapers

Afisa wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Afariki Dunia Katika Mazingira ya Kutatanisha

0
Msimamizi wa uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya kwenye jimbo la Gichugu, Geoffrey Gitobu

 

Afisa wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya, Geoffrey Gitobu amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha, zikiwa ni siku chache tangu kufanyika uchaguzi mkuu.

 

Gitobu ambaye alisimamia uchaguzi katika Jimbo la Gichugu, amefikwa na mauti ya ghafla jana Jumatatu, Agosti 23, 2022.

 

Kamanda wa Polisi wa Laikipia, John Tarus ameliambia Gazeti la The Nation kwamba kifo hicho kimeripotiwa na kaka wa marehemu Jumatatu mchana.

 

Kamanda huyo ameeleza kuwa kaka wa marehemu aliripoti kuwa ndugu yake alikuwa akiendesha gari katika Mji wa Nanyuki ambapo ghafla alianza kujisikia vibaya kikiwemo kizunguzungu kikali, akakimbizwa hospitali lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya mpaka alipofikwa na mauti.

 

Kamanda huyo wa polisi ameeleza kwamba kaka wa marehemu alipohojiwa amesema ndugu yake hakuwa na tatizo lolote la kiafya na kwamba alifia katika Hospitali ya Cottage alikofikishwa baada ya kuzidiwa ghafla.

 

Inaelezwa kuwa afisa huyo wa tume ya uchaguzi, alikuwa mfanyabiashara maarufu katika Mji wa Nanyuki ambako anamiliki majengo kadhaa ya biashara.

 

Taarifa za kifo cha Gitobu, zimethibishwa na Meneja wa Uchaguzi wa Kirinyaga, Jane Gitonga ambaye amesema uchunguzi wa mwili wa marehemu, utafanyika ili kubaini chanzo cha kifo chake.

MKE WA MREMA AISHIWA NGUVU MWILI WA MUMEWE UKIWASILI NYUMBANI..

Leave A Reply