The House of Favourite Newspapers

Steve Nyerere ‘Asusa’ Msiba wa Mzee Majuto: Sihusiki na Chochote – Video

MUIGIZAJI Steve Nyerere ambaye amekua mstari wa mbele kuwaunganisha wasanii hasa katika kipindi cha misiba au matatizo yanayowatokea wasanii wenzao, amesema hahusiki chochote na kuwakuwaweka pamoja wasanii wenzake kwani amekuwa akitukanwa kwamba anakusanya pesa rambirambi kisha ‘anazitafuna’.

 

Steve amekua akitukanwa na baadhi ya watu na mastaa wenzake kutokana na kuonekana mara nyingi kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli mbalimbali hasa za misiba ambapo amesema katika msiba wa Mzee Majuto yeye ni muombolezaji kama waombolezaji wengine hivyo hahusiki na chochote.

 

Mzee Amri Athumani aliaga dunia jana usiku majira ya saa 2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akitibiwa, anatarajiwa kuagwa leo Karimjee na kusafirishwa kwenda Tanga kwa maziko.

 

MSIKIE STEVE AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.