The House of Favourite Newspapers

Michirizi Ya Damu – 08

0

Akakaa na kumsubiria mzee huyo. Alimwambia kwamba angefika nyumbani hapo muda si mrefu. Akajiachia kochini huku moyo wake ukiwa na amani kwamba alifanikiwa kulala na Dk. Fabby, hata kama hakumtaka tena kwake wala hakulijali sana.

Baada ya saa moja, Keith akafika nyumbani hapo. Alipomuona Fareed, akamfuata na kumkumbatia. Alimkumbuka na muda wote alikuwa akimuwaza yeye tu. Walikaa na kuzungumza, Keith hakutaka kumwambia ukweli Fareed jinsi alivyokuwa akijisikia ila alijua kwamba mwanaume tata huyo alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Umefanikiwa?” aliuliza Keith.

“Ndiyo!”
“Safi sana, hebu nione,” alisema mwanaume huyo na kutaka kuonyeshewa.

Hilo halikuwa tatizo kwa Fareed, akavua nguo zake na kisha kumwangalia. Mapigo ya moyo wa Keith yalikuwa yakienda kasi, hakuamini kama alikuwa akimwangalia mwanaume huyo.

Mwili wake ukamsisimka, hakutaka kukubali, akamchukua Fareed na kwenda naye kitandani, hapo, akaanza kumwambia maneno mengi ya mahaba, jinsi alivyokuwa akimpenda, hakuacha kumsifia kwa kila kitu kiasi kwamba Faredd akajiona kuwa mzuri kuliko watu wote duniani.

“Kweli?”
“Ndiyo! Wewe ni malaika wangu, ni mrembo kuliko warembo wote waliowahi kutokea katika hii dunia!” alisema Keith maneno ambayo alikuwa na uhakika kwamba hayakuwa kweli bali alitaka kukamilisha kile alichokitaka.

Fareed akaachia tabasamu pana, akajiangalia, akahisi kwamba kweli alikuwa mrembo kuliko warembo wote waliowahi kutokea katika dunia hii. Akashikwa mkono, akaacha, akashikwa bega, akaacha, kila alipokuwa akishikwa huku na kule, aliacha na mwisho wa siku, baada ya saa moja wote kujikuta wakiwa hoi kitandani.

“Ahsante,” alisema Fareed huku akimwangalia Keith kwa uso uliokuwa na tabasamu pana.

“Umeridhika?”
“Sana mpenzi! Kumbe nilikuwa najichelewesha tu!” alisema Fareed huku akimwangalia mwanaume huyo.

Penzi jipya likaanzishwa, kila mmoja alikuwa bize na mwenzake, japokuwa Keith alikuwa na familia yake jijini New York lakini hakutaka kurudi huko, alitekwa na biashara zake zote alizihamishia huko, mahesabu akawa anapelekewa hukohuko alipokuwa.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, mapenzi ya jinsi moja yalimpeleka puta na hakukumbuka kitu chochote kile. Siku wiki moja baadaye akaamua kumfanyia sapraizi Fareed, alitaka kumnunulia gari jipya kwani hakutaka kuona akipata tabu yoyote ile.

Siku hiyo akakaa na kuzungumza naye mengi, ilipofika saa sita mchana, akamchukua na kisha kuondoka nyumbani hapo. Wakati wametoka ndani ya jumba hilo kubwa na kushika barabara, ghafla akaliona gari moja likiwafuata kwa nyuma.

Wakawa na hofu kwa kuhisi kwamba inawezekana watu waliokuwa humo walikuwa majambazi waliotaka kuwaua au kuwaibia hivyo. Kila Keith alipokuwa iongeza mwendo, gari la nyuma likawa linaongeza kasi kiasi kwamba wakaona huo ndiyo ungekuwa mwisho wao.

Walichokifanya ni kuingia kwenye barabara kubwa ambapo walikwenda mpaka sehemu iliyokuwa na watu wengi, akalisimamisha gari hilo kwa kuamini kwamba hata kama watu hao wangeteremka kwenye gari na kuwafuata, wasingeweza kuwaua kutokana na wingi wa watu mahali hapo.

Gari lile la nyuma likasimama na mwanaume mmoja kuteremka. Hawakuzungumza kitu, walibaki wakimwangalia mwanaume huyo ambaye alionekana kuwa na hasira kubwa.

Fareed hakumtambua mpaka alipofika karibu, Keith akateremsha kioo, macho ya Fareed yakatua kwa mwanaume aliyekuwa akimfahamu, alikuwa Godfrey aliyeonekana kuwa mwenye hasira kupita kawaida.

Akaanza kuwaangalia wote wawili kwa macho yaliyokuwa na shari, kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa tayari kufanya jambo lolote lile kwani hata mwili wake ulianza kutetemeka kwa hasira kali.

****

“What can I help you, sir?” (nikusaidie nini bwana mkubwa?) aliuliza Keith huku akimwangalia Godfrey aliyekuwa na hasira kali.

“I want my bae,” (namtaka mpenzi wangu)

“Your bae? Who the hell is she?” (mpenzi wako? Ndiye nani huyo?) aliuliza Keith huku akimwangalia mwanaume huyo machoni.

Godfrey akayahamisha macho yake na kumwangalia Fareed ambaye alikuwa akitetemeka tu. Kwa kitendo kile cha kumwangalia Fareed, Keith akajua mtu aliyekuwa akizungumziwa na hivyo kumuuliza Fareed kama alikuwa akimfahamu mwanaume huyo.

“I don’t know him,” (wala simfahamu) alisema Fareed huku akimwangalia Godfrey kwa macho yaliyojaa mshangao, alionekana kama kweli hamfahamu mwanaume huyo.

“Fareed, look at my eyes! Don’t you know me? Look at my eyes bastard,” Fareed, yaangalie macho yangu! Hunifahamu? Yaangalia macho yangu mwanaharamu weee) alisema Godfrey huku akionekana kuwa na hasira kali zaidi.

Bado Fareed aling’ang’ania kwamba hakuwa akimfahamu mwanaume huyo na hiyo ndiyo siku ya kwanza kumuona machoni mwake. Keith hakutaka maswali zaidi, alichokifanya ni kumwambia dereva wake aliondoe gari mahali hapo na kufanya hivyo.

Godfrey alibaki akiwa amelowa, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea, kukataliwa na Fareed mchana kweupe namna ile kulimuumiza mno moyoni mwake. Watu wote walikuwa wakimwangalia, wengine walimpigia honi kumaanisha kwamba walimtaka aondoke mahali pale ili waendelee na safari yao.

Akarudi ndani ya gari, akaingia na kutulia kwenye usukuni, alikuwa na wazo tele na muda mwingine alikuwa akitokwa na machozi, kwa kile kilichokuwa kimetokea kwake kilionekana kuwa kama ndoto ya mchana. Hakukaa sana mahali hapo, akaondoka zake huku akiwa na hasira kifuani.

Moyo wake ukajaa ghadhabu, hakufikiria kitu kingine kama kumuua Fareed. Aliutesa moyo wake, hakuwa radhi kumuona mwanaume tata huyo akiendelea kuishi na wakati aliuumiza moyo wake kupita kawaida.

“Ni lazima nimuue, nitatumia gharama zangu zote kumuua huyu mpumbavu,” alisema Godfrey huku akionekana kuwa na hasira sana. Moyo wake ukapanga kumuua Fareed kama kumlipizia kisasi kwa kile alichokifanya.

***

Wanaume wote waliokuwa wakitembea na Fareed walichanganyikiwa, hawakuamini kama alikuwa akijua sana kitandani. Mioyo yao iliuchanganyikiwa, walipokutana naye, hawakutaka kumuacha, waliendelea kumtafuta zaidi na zaidi.

Kitendo cha kuwa na Keith kwake yalikuwa mateso makubwa, alibanwa sana kwani mwanaume huyo hakutaka kumuona akiondoka kuelekea sehemu yoyote ile.

Alipokea simu kutoka kwa matajiri wengi ambao walimuahidi kumpa kiasi kikubwa cha fedha lakini kuonana nao suala hilo lilikuwa gumu sana. Aliwasiliana nao kwenye simu, aliwatumia picha zilizokuwa zikionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa mzuri.

Hakuzoea kuwa na mwanaume mmoja, tangu alipompata wakala wake, Asteria, alikuwa akitoka na wanaume mbalimbali, hayo ndiyo yalikuwa maisha yake na hata alipoambiwa na Keith kwamba hakutakiwa kutoka, kwake yalikuwa mateso makubwa.

“Haiwezekani! Siwezi kukaa na mwanaume mmoja, kwani kanioa? Yeye mbona ana familia yake, lazima nitoke,” alisema Fareed huku akionekana kutokukubaliana na kile kilichokuwa kikiendelea.

Ndivyo alivyofanya, baada ya wiki moja huku akiwa amempa Godfrey mahaba mazito akaamua kuondoka na kuelekea Dubai. Hakuwa ameaga, alimtoroka kwani kitu alichokuwa akikiangalia ni kwa namna gani angeweza kuifurahisha roho yake.

Huko Dubai alikwenda kuonana na bilionea mwingine, Saed ambaye alikuwa akimsumbua sana kwenye simu. Walipoonana kwa mara nyingine, wakaelekea kitandani ambapo huko wakafanya mambo yote na kukumbushiana siku ya kwanza walipokuwa wameonana.

Hakutaka kuwasiliana na Keith, mwanaume huyo alimpigia sana simu kutaka kuzungumza naye lakini hakupokea, alinyamaza kimya na hata zile meseji alizokuwa akitumiwa, nazo hakuzijibu japokuwa aliziona na kuzisoma.

Akili na mawazo yake yalikuwa kwa Bilionea Saed tu ambaye hakuwa msiri, alimchukua Fareed na kumtamulisha kwa baadhi ya marafiki zake na kuwaambia kwamba alikuwa mpenzi wake wa kufa na kuzikana. Hilo lilimpa furaha Fareed kwa kuamini kwamba angeishi milele na mwanaume huyo.

Marafiki wa Saed nao hawakutaka kukubali, kwa kuwa Fareed alionekana kuwavutia tena huku kwa nyuma akianza kutuna na kifua kuonekana, hawakutaka kumuacha, walichokifanya ni kuanza kummendea kitu ambacho kilimfurahisha kwani akili yake ilifikiria fedha kuliko mapenzi.

Alipokea meseji nyingi kutoka kwa wanaume mbalimbali, wote walimtaka kimapenzi. Hakuwa mchoyo, alikubali kufanya nao na hivyo kukutana nao sehemu yoyote waliyotaka na kuwaridhisha.

Ndani ya mwezi mmoja akatembea na marafiki kumi wa Saed, hakuwa akijua, alipokuwa naye alikuwa akimsifia kwa marafiki zake kumbe ndiyo haohao waliokuwa wakimbadilikia kila alipowapa kisogo.

Wakati mwezi wa pili ulipokatika, ndipo akaingia kwenye umbo rasmi la kike, alikuwa na muonekano kama wa wanawake wengine, alikuwa na kifua kikubwa, wowowo, mavazi ya kile, alijitahidi kuibadilisha sura yake kwa kuipaka sana poda, akaseti nywele zake, kwa kifupi alikuwa mwanamke kamili isipokuwa sehemu za siri ambapo alishindwa kuibadilisha.

“Hivi huyu mpumbavu Keith anaendelea kunisubiri au? Asahau! Mimi siwezi kuwa na bwana mmoja. Kwanza ukila ugali kila siku utachoka, siku nyingine kula wali, ukiuchoka, kula pilau, nalo ukilichoka, nyonya koni,” alijisemea huku akiirambaramba midomo yake kama mwanamke aliyepewa ahadi ya kukutana na mwanaume kwenye nyumba ya wageni.

Wakati yeye akifikiria hayo yote, upande wa pili Keith alikuwa na hasira kali, hakuamini kama kweli Fareed alikuwa amemtenda kiasi hicho na wakati alikuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha kumgharamia.
Hakukubali, moyo wake ulijaza ghadhabu nzito na alikuwa tayari kufanya lolote lile kumshughulikia mwanaume huyo.

Alimtafuta, aliwaagiza vijana wake kila kona hapo Los Angeles kumtafuta na kumleta kwake. Vijana hao wakafanya kazi usiku na mchana, wakazunguka katika Cassino mbalimbali lakini hawakuweza kumuona. Hawakuishia hapo, wakazunguka kwenye miji mingine lakini napo hawakuweza kumuona kitu kilichowapa maswali mtu huyo alikuwa wapi.

“Tumemtafuta sana! Hatujamuona!” alisema kijana mmoja.
“Sawa. Ngoja nimpigie wakala wake,” alisema Keith na kumpigia simu Asteria, alitaka kufahamu mahali alipokuwa Fareed ili amuue, hata mapenzi aliyokuwa akiyataka, yakamtoka, hakuwa radhi kuona mtu aliyemgharamia akimchukua mwanaume mwingine.

“Na akisema yupo Tanzania tu, namfuata na kumuua hukohuko!” alisema Keith na kumpigia simu mwanamke huyo. Kwa kuwa Fareed hakumwambia kuhusu kumtoroka Keith, wala kumwambia kwamba alikuwa bwana wake mpya, mwanamke huyo akamwambia kwamba alikuwa Dubai akila maisha na bilionea Saed, maneno yaliyomchoma mno Keith.

“Yaani anakula maisha na mwanaume mwingine. Sasa atanitambua,” alisema Keith! Hapohapo akawapigia simu vijana wake. Alitaka kuzungumza nao, mezani kulikuwa na jambo moja tu. Kumteka Fareed na kumuua.

***

Huko Dubai maisha yalikuwa ni ya raha kabisa, Fareed hakuishia kwa wanaume hao tu, alichokuwa akikiangalia kilikuwa pesa tu. Siku zikakatika huku akiendelea kupata fedha, alilala katika mahoteli makubwa na ya kifahari ambayo alipangiwa na mabwana zake.

Alisahau kabisa kama kulikuwa na shida katika dunia hii, alifurahia kwa kuwa aliona kwamba hakukuwa na kitu alichoshindwa kukifanya kwa sababu alikuwa na pesa ya kufanya kitu chochote kile.

Baada ya wiki mbili akapigiwa simu na mwanaume mmoja, alikuwa mwanaume wa Kizungu aliyemwambia kwamba alitaka kuonana naye, mwanaume huyo alijitambulisha kwa jina la Mickey Downford.

Kwanza Fareed hakutaka kukubali, lilikuwa jambo gumu kukutana na mwanaume huyo, alihisi kwamba hakuwa na fedha za kumpa kwani yeye aliwazoea mabwana wa Kiarabu ambao walikuwa radhi kutoa kiasi chochote cha pesa ili kupata wanachokihitaji.

Kwa kipindi cha wiki nzima Mickey alikuwa akiomba kuonana na Fareed lakini alikuwa akikataa na wakati mwingine alimwambia kwamba hakuzoea kutembea na Wazungu, yeye aliwapenda Waarabu tu.

“Lakini nina pesa!” alisema Mickey kwenye simu.

“Nitaamini vipi?”
“Subiri! Nipe namba yako ya benki,” alisema Mickey na hivyo kupewa namba hiyo.

ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA

Leave A Reply